Maramba ndio kwetu, ulichoandika ndio ukweli. Kinachosababisha hali kama hiyo ni uongozi, lazima wana mkinga tusiwe waoga tuwe wawazi kwamba hata kabla halijagawanyika toka muheza mpaka sasa jimbo la mkinga hatujawahi kupata mbunge mbunifu na mwenye uchungu wa maendeleo ya wengine.
Wote ni walalavi wa fikra hawawezi hata kutangaza uzuri, umuhimu na faida ya rasilimali zilizopo hapo.Mkinga kuna ubunge wa kifalme. Akitoka "ndula" anaingia "kita" tuamkeni wana Mkinga, kama hatuwezi kuwatoa basi tuwakemee au hata kuwakatalia kuwazomea kwa madhaifu yao.
Kwa upande wangu nawakataa wala sioni cha kunishawi toka kwao.Wataniambia nini najua ni wezi na wabinafsi kwa kuwa kwetu kuna "hifadhi ya misitu, milima,hifadhi ya wanyama,bahari za fukwe, bahari za uvuvi,bahari za usafirishaji, Tanga stones, madini ya aina zote, kilimo cha mkonge, karafu, sufi, kakao na mazao ya chakula na mengineyo kama ardhi yenye rutuba, cha ufundi, kambi ya jeshi, chuo cha uhamiaji na ndio mpaka na nchi jirani ya kenya. Kataa umasikini wa kujitakia. 2025 itei