Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Hayo yamebainishwa leo Agosti 20, 2024 na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde wilayani Tarime mkoani Mara wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mfano wa hundi tano za malipo ya mirabaha kwa vijiji vitano kutoka katika mgodi wa dhahabu wa North Mara.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde
Akielezea kuhusu ushirikishwaji wa Vijana , Wakina mama na Wazee katika sekta ya madini eneo la Nyamongo , Waziri Mavunde ameigiza Tume ya Madini kupitia Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Tarime kushirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Mara kutenga maeneo maalum yatakayofanyiwa utafiti na kugawiwa kwa makundi hayo kwa ajili kufanya uchimbaji wenye tija.
Akifafanua kuhusu mpango wa utekelezaji wa Maudhui ya Ndani (Local Content), Waziri Mavunde amesema , Wizara ya Madini itashirikiana na Wizara ya Kilimo kwenye mradi wa uchimbaji visima vya maji kuchimba visima katika eneo la Nyamongo ili kuongeza fursa ya upatikanaji wa maji kwa kilimo cha mbogamboga kama walivyoanza.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa NorthMara, Apolinary Lyambiko
Lyambiko amevitaja vijiji hivyo nufaika kuwa ni pamoja na Kerende, Kewanja, Nyamwaga, Nyangoto na Genkuru. North Mara Gold Mine Limited imeendelea kutoa gawio la Mrabaha kwa vijiji 5 ambavyo vilikuwa vikimili maeneo yenye leseni za uchimbaji (PML) wakati mgodi unaanzishwa na Kampuni ya Afrika Mashariki Gold Mines Limited (Sasa North Mara Gold Mine Limited) mnamo tarehe 27 April 1996
Lyambiko ameongeza kuwa, kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2020 hadi 2024 kiasi cha bilioni 69 kimelipwa kwa Serikali ikiwa ni malipo mbalimbali yanayotokana na Mgodi.
Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe.Masache Kasaka ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya madini hususani kwenye uwazi katika utoaji wa mirabaha.
Nae, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja. Edward Gowele ameipongeza Serikali kupitia wizara ya madini kwa kazi nzuri inayofanya katika kushirikisha jamii kwenye miradi ya kitaifa ikiwa ni mipango na mikakati ya kuwanufaisha kwenye rasilimali zinazowazunguka katika maeneo yao na kuhaidi kushiriki kikamilifu katika utatuzi wa migogoro yote iliyopo katika wilaya ya Tarime.
Akizungumza kwa niaba ya Mbunge wa Tarime Vijijini, Lemi Mkapa ameishukuru Serikali kwa kuwajali wananchi wa Nyamongo kwa kuweka mpango wa wazi katika utoaji wa mrabaha ambapo kupitia fedha hizo jamii itaibua miradi ya kijamii na kutatua changamoto zilizopo.