Kwani wamasai hawaishi kwa muingiliano na wanyama katika mbuga zingine zozote ila Ngorongoro crater hadi iwe unique factor ya watu kwenda kuitembelea ??...
Kwa ukubwa wa Ngorongoro na ikolojia yake unadhani hii haitoshi kuwafanya watu kuitembelea ??..
Leo tukisema tukimege kipande cha ruaha au mikumi ili kitumike kwa shughuli za kibinadamu bado kuna serengeti au selous inayotoa same experience Je, tukiiweka Ngorongoro crater hatarini kuna option gani nyingine tuliyonayo kui_replace
Ngorongoro haikumegwa ili Wafugaji wapate mahali pa kuishi.
Kilichotokea, tangia miaka ya 1920, baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia, alipoondolewa Mkoloni Mjerumani akaja Mkoloni Muingereza, Wazungu walishangaa walipofika Ngorongoro na kukuta Wafugaji wanaishi na Wanyamapori pamoja.
Hali hiyo iliwavutia sana, wakaazimia hali hiyo iimarishwe na kudumishwa.
Na sababu kubwa ni kwamba Wamasai hawali nyama ya Wanyamapori.
Wanakula nyama ya mifugo yao, ambayo ni Ng'ombe na Mbuzi.
Na hii, kwa kweli, ni 'unique'.
Kwa hiyo kuwaondoa Wafugaji hao Ngorongoro, ni kuwaondoa nyumbani kwao.
Itakuwa ni dhuluma.
Wataalamu, katika Tafiti zilizofanyika, wanasema kinachoiharibu Ngorongoro ni Ujenzi holela unaochochewa na ulaji RUSHWA kwa watoa vibali vya Ujenzi ambao ni Ngorongoro Conservation Area Authority, NCAA. (Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro).
Tatizo ni Mamlaka, siyo Wafugaji.
Wakati namshukuru Maulidi Kitenge kwa kuibua Mjadala huu, wanaomlaumu pia wanayo hoja.
Kwa nini hakueleza Uzembe wa Mamlaka ya Hifadhi ambao wanakula marupurupu manono huku hii World Heritage ikianza kuteketea?
Wahifadhi wa kweli ni Wafugaji Wamasai.
Wapongezwe sana.
Wasibezwe.
Mamlaka ndiyo iwekwe kwenye Kitimoto.