Mgogoro Hifadhi ya Ngorongoro kuna siri nzito. Nani wapo nyuma ya Wamasai?

Kuna watu wanakurupuka sana humu , uniqueness ya ngorongoro ni pamoja na wanyama kuishi na watu bila kudhuriana hii ndio maajabu yenyewe yani wana mambo yao ambayo wamekubaliana sasa ukiondoa kimoja wapo ule umaana wa hilo bonde haupo. Mnamsikiliza mshambuliaji mzee wa uno as if hoyo ajenda ni yake? yule katumwa tu ukiona ngedere mjini ujue kafugwa na wenyewe wapo tena karibu tu
 
Ngorongoro haikumegwa ili Wafugaji wapate mahali pa kuishi.
Kilichotokea, tangia miaka ya 1920, baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia, alipoondolewa Mkoloni Mjerumani akaja Mkoloni Muingereza, Wazungu walishangaa walipofika Ngorongoro na kukuta Wafugaji wanaishi na Wanyamapori pamoja.
Hali hiyo iliwavutia sana, wakaazimia hali hiyo iimarishwe na kudumishwa.
Na sababu kubwa ni kwamba Wamasai hawali nyama ya Wanyamapori.
Wanakula nyama ya mifugo yao, ambayo ni Ng'ombe na Mbuzi.
Na hii, kwa kweli, ni 'unique'.
Kwa hiyo kuwaondoa Wafugaji hao Ngorongoro, ni kuwaondoa nyumbani kwao.
Itakuwa ni dhuluma.
Wataalamu, katika Tafiti zilizofanyika, wanasema kinachoiharibu Ngorongoro ni Ujenzi holela unaochochewa na ulaji RUSHWA kwa watoa vibali vya Ujenzi ambao ni Ngorongoro Conservation Area Authority, NCAA. (Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro).
Tatizo ni Mamlaka, siyo Wafugaji.
Wakati namshukuru Maulidi Kitenge kwa kuibua Mjadala huu, wanaomlaumu pia wanayo hoja.
Kwa nini hakueleza Uzembe wa Mamlaka ya Hifadhi ambao wanakula marupurupu manono huku hii World Heritage ikianza kuteketea?
Wahifadhi wa kweli ni Wafugaji Wamasai.
Wapongezwe sana.
Wasibezwe.
Mamlaka ndiyo iwekwe kwenye Kitimoto.
 
Shida wamasai wakihama utaona ndege za kiarabu na mihoteli inajengwa. Ni lini mnyama alimzidi binaadam hadhi. Mnasema wanyama wanahatarisha maisha ya wamasai mbona mnakiri kuongezeka kwa uzao wao. Tatizo watu wa kiuongozi wa kitanzania hawaaminiki .na hapa ndo pakuanzia waweza kuta hao wanyama wanaotetewa wakavunwa kama mahindi. Na watakaohamishwa wakakosa hata mavazi huko watakapohamia. NAeneo lenyewe wakapewa wazito fulani wa kidunia kutamba. ALIEMFANANISHA MWAFRIKA NA NYANI ALIONA NINI? MAANA HILI TUSI KUNA WAKATI LINASWIHI KABISA.
 
Nchi hii ardhi yote ni mali ya umma iko chini ya mamlaka ya Rais wanaojidai kuwaambia wamasai kuwa ngorongoro ni kwao na haiwezekani wao kuondoka wajue wanawadanganya
Yawezekana kweli Ardhi yetu ni Mali ya Raisi lakini hata wewe hapo ulipo utakuja kuhamishwa kwasababu serikali ina hitaji Ardhi hiyo Kwa Matumizi mengine!!..Utalii wa Ngorongoro ni kwasababu ya binadamu wanaoishi na wanyama Pori,kuna siku mtakuja kusema kule Saadani tuwaondoe wanyama kwasababu watu wanajenga Kwa speed sana Kijiji cha Kitame!!
 
Ile nyumba haikai tu wamaasai wako wambulu, wachaga, wakikuyu,wameru nk! Tatizo ni nyumba imejaa kupindukia na kila mtu ana interest zake pale!
Kuna cross breeding ya kufa mtu pale na mchanganyiko wa tamaduni za kutosha hivyo ni ngumu sana hawa ormaasinda kudumisha mila kama awali! Unategemea nini mfanyakazi Mmaasai wa NCAA ameoa mchaga au mpare au mmeru au msukuma waishi kwenye tembe!? Wasifungue kaduka au ka grocery na amapiano zikatumbuiza wildlife kupitia sabufa!!😂😂
Nashauri tu itungwe sheria ni kilometa ngapi raia anayestahili asiishi katika zone flani Dili kupunguza muingiliano wa kibinadamu na wanyama pori! Ujenzi wa hizi lodge umepindukia! Kwanza ndio unaleta population ndani ya hifadhi na kuufanya utalii kuwa wa ghali mmno na uharibifu wa nature! Wawekezaji waanze kuwekeza mahoteli nje ya hifadhi watu watafuata ajira huko! Kuwe na utaratibu wa kubalance namba ya waajiriwa hii itapunguza msongamano ndani ya hifadhi! Serikali iweke kiwango cha mifugo mzawa anachotakiwa kuwa nacho, wapewe first priority soko la nyama kwa hoteli zilizopo ndani ya hifadhi, hii itapunza idadi ya mifugo ndani ya hifadhi!
Hivi serikali mkiamua kuhakikisha Karatu, makuyuni na njia ya Engaruka to lake natron kuwa ni ukanda wa malazi ya aina zoote hamuoni itawachomoa watu mahali!? Jengeni sekondari na primaey za bording nje ya hifadhi!
Binadamu halazimishi aishije ila mazingira yakimvutia anajiongeza mwenyewe!
Jamani! Ni maoni tu na ushauri hapingwi kwa kupigwa rungu!
 
Mtaondoka tu
 
Kuwe na kiwango maalum cha wakazi siyo kama sasa laki mbili
 
Acha ujinga. Waanze kwanza kwa kubomoa na kukataza ujenzi wahoteli ndani ya hifadhi. Kipi kinaharibu hifadhi kati ya Hoteli kubwa ya nyota 5 ya kitalii na tembe zetu za nyasi?
Pili: Swala la huduma za jamii, tunaweza kuzifuata mbali, sio lazima zijengwe pale hifadhini. Hatuondoki.
 
Kwa hiyo Masai tumconserve kwa kuwa ni mifugo sio?
 
Umaarufu wa eneo hilo ni kuwa Hifadhi pekee yenye matumizi mseto (jamii na wanyamapori). Sifa hii imeifanya kuwa moja ya majabu ya Dunia. Hali hii imechagizwa na tamaduni, Mila na desturi ya kabila la kimasai ambao enzi na enzi wamekuwa rafiki na wanyamapori, sote ni mashahidi.

Hoja ya wahifadhi kutaka kuondoa wamasai ni madai ya ongezeko la watu na mifugo kitu ambazo kitaalam bado hawaja tuweka sawa kwa maana ya kuja na taarifa za kitaalam hususan Carrying capacity. Ukiachilia mbali idadi ya watu nimeona ripoti mbalimbali zikionyesha idadi ya mifugo kupungua badala ya kuongezeka.

Kitenge na wenzake wameripoti maisha ya umaskini na ufukara kwa jamii Ile, hili linanipa mashaka kuwa management ya eneo hilo hawatekelezi yale malengo matatu (Uhifadhi, Utalii na Kuendeleza jamii) kwa usawa. Eneo hili linakusanya zaidi ya bil. 160 kwa mwaka, how come zaidi 97% ya jamii pale wanakuwa fukara na maskini kwa population ya watu elfu 70? ikiwa NCA ni moja ya ma giant ya mashirika ya umma nchini?

Hii pia inanipelekea kuamini kwamba huenda Uhifadhi Shirikishi inayohimiswa na Dunia ya sasa haifanyiki pale. Kujumuisha Uhifadhi na miradi ya maendeleo ni moja ya mbinu inayohimiswa na wataalam wahifadhi duniani ktk kufikia Uhifadhi Endelevu, mbinu hii itakidhi mahitaji ya jamii na kupunguza utegemezi kwa rasilimali za asili. Jamii huenda hawashirikishwi kikamilifu ktk usimamizi wa eneo hilo kwa ngazi zote, huenda jamii hawawezeshwi miradi mbadala rafiki na uhifadhi. Lakini pia management huenda hawana programs nzuri ya kuboresha mifugo, kuweka masoko, viwanda ya mazao ya mifugo na utengwaji na uboreshaji nyanda za Malisho.

Huenda pia utoaji Elimu ya Uhifadhi kwa jamii ni hafifu ndani ya eneo hilo. Elimu kwa jamii Ile ingetosha kuwa tool mojawapo ya kupunguza watu pale watasoma na wengi wao watafanya kazi nje ya pale. Yote haya ni ya kutazamwa na Mamlaka za juu na sisi wadau Ili tuweze kushauri.
 
Ni kweli ndugu ila kueneza propaganda siyo njia sahihi ya kutatua changamoto.
 

nilimuuliza ili ajue kuwa Ngorongoro si sawa na sehemu nyingine kama alivyokuwa akiielezea, Ngorongoro ni unique kwa hiyo haina replacement

Ahsante pia kwa kunipa maelezo mazuri mkuu, kama shida ni watu wanaoifanya kuwa modern badala ya kuwa katika uhalisia wake kimuingiliano na wanadamu, bhasi waangalie njia bora ya kuirejesha ile asili yake
 
Umeandika vizuri sana.
Wahifadhi wa kweli Ngorongoro ni Wafugaji wa Kimasai.
Hawawindi Wanyamapori.
Hawali nyama ya Wanyamapori.
Waharibifu wa Ngorongoro ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Ngorongoro Conservation Area Authority, NCAA.
Mamlaka inafanya makusudi kuhamishia lawama kwa Wafugaji ambao wameishi na Wanyamapori kwa miaka na miaka.
Tatizo la Ngorongoro ni Mamlaka.
Tatizo ni NCAA.
 
Mkuu, hapo Ngorongoro Kuna NGOs kama 1,000.

Zote zinamwagiwa pesa kutetea Masai waendelee kuwepo Hapo.

Huo Ni mradi wa watu wengi sana wakiwemo wapiga kelele.

Hata wewe anzisha NGO yako ya mfukoni iwe based on Ngorongoro, huwezi kukosa Donor.
 
Swala la ngorongoro liko wazi mengine ni siasa tu na hoja zakuokoteza.Naona kuna ambao wanasema ngorongoro ni unique kwasababu ya binadamu wanaoishi uko ndani hiyo ni hoja mfilisi kabisa.kwasababu swala la binadamu kuishi na wanyamapori ni kawaida kabisa na haijawai kua ngorongoro tu.Serengeti walishawai kuhamishwa wanajijiji,lakini pia kuna kijiji cha ikoma rubanda bado wanyama wanafika hadi kwenye makazi ya watu.ukienda saadani kuna vijiji viko hifadhini na maisha yanaendelea wala hakuna la ajabu kwenye hilo.Tatizo la ngorongoro ni wananchi kubadilika tabia na idadi ya wananchi kuongezeka tofauti na mwanzo wakati sheria yakuwaruhusu wakae inapitishwa.ata ivyo shughuli za kiuchumi za wananchi hao zinahatarisha uwepo wa hifadhi kwasababu ya ongezeko kubwa la idadi ya mifugo.Binadamu wanapoongezeka na mahitaji yanaongezeka lakini pia mifugo nayo inaongezeka kwahiyo lazima itafika kipindi hali itakua mbaya zaidi.kama nchi inajielewa hichi sio kitu chakuchelewa kuchukua hatua.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Survival of the fittest si ndiyo!
 
Sio mbaya ila ifike wakati binadamu awe na thamani kuliko mnyama, wangehamishwa wanyama binadamu wakaishi na sioni kama kuna tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…