Mgogoro Hifadhi ya Ngorongoro kuna siri nzito. Nani wapo nyuma ya Wamasai?

Mkuu hizi agenda watu hawasukumi bure... kuna pesa nyingi sana watu wanavuta kutoka kwa foundations mbalimbali duniani.

Angalia NGO ya Maria Sarungi ililipewa pesa kiasi gani mwaka 2018



Unaweza kujikuta unasukuma gari la wenzako bila kujua. Ndio maana watu wengi mtandaoni wakianza kupiga kelele kuhusu jambo moja wanageuka kama makasuku, maneno yaleyale na inawezakana yanaandikwa na mtu mmoja
 
Hao wanaopinga kutolewa kwa wamasai ni Wakenya wanaotaka kuiua Ngorongoro ili vivutio vinavyoleta ushindani na vile vya Kenya vipungue Tanzania. Bahati mbaya wamasai wa kenya ni sawa sawa na hawa wa Tanzania hivyo inaweza kuwa ni mamluki wao pia.
Ni kweli kabisa mkuu. Kuna tetesi kuwa hii hifadhi yetu inahujumiwa
 
wamasai wanatumika kuweka mifugo ya vigogo tu vigogo wan ngo'mbe kibao zinakul nafasi za hifadhi,ngo'mbe laki 8 huku kati ya hiyo no 3% tu ndio za wamasai.
 
tatizo siyo wamasai bali kuna vigogo wameweka mifugo kwenye Hitadhi wakiwatumia wamasai.
 
It's a matter of time mtatoka tu mtake msitake....watu laki 2 mnatoa wapi kuni za kupikia kila siku? Kama sio kuharibu mazingira? Msituletee habari ya miaka 70 iliyopita!
 
Ni kweli kabisa mkuu. Kuna tetesi kuwa hii hifadhi yetu inahujumiwa
Hii hifadhi inahujumiwa kabisa na ni rahisi kufanya hivyo kutokana na umbo lake na udogo wake ukilinganisha na Serengeti iliyopakana na Masai Mara. Nilifanya utafiti kidogo ndani ya hifadhi hii nikaona kuwa hata mimea imeanza kuota ambayo sio mimea ya asili, sasa unajiuliza wanyama wataendelea kuwepo pale kwa hali hii? Je ni nani ameleta mbegu hizi kama sio hawa binadamu wema na wenye nia mbaya wanaojificha nyuma ya sheria ya kikoloni? Hivi sisi Tanzania si tulipinga sheria ya kikoloni ya kugawa mpaka ziwa Nyasa? sasa inakuwaje huku tunafumbia macho mbuga ambayo inapata tuzo za utalii za kimataifa?
ANALYSIS
Tanzania yenye eneo kubwa 945k sq km ni zaidi ya eneo ukijumlisha Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda 875k sq km. Population ya Tanzania ni 60m lakini ya Kenya 54m, Uganda 46m, Rwanda 13m na Burundi 12m inafanya jumla kuwa 125m. sasa ukiondoa 30% ya ardhi ya Tanzania ambayo ni hifadhi na mapori ya akiba, population density ya Tanzania inakuwa 91 people per sq km, wakati ya Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kwa pamoja bila kuondoa hifadhi na mapori ya akiba ni 143 people per sq km. Hivyo wenzetu wana pressure ya maeneo kuliko sisi. ndio maana mbuga zetu zimebaki bora kwa sababu hazina muingiliano mkubwa na watu. sasa upenyo uliopo NCAA ndio wanataka kuutumia kutudhoofisha, tuamke!
RECOMMENDATION
Sheria ya kuruhusu makazi ndani ya Ngorongoro ifanyiwe mrekebisho ili wakaazi ndani ya NCAA wahamishwe kisheria, kwa vyovyote vile zoezi litapingwa lakini serikali ina mkono mrefu izuie kuhujumiwa.
 
Wizara ya Maliasili iharakishe kupitia sheria ya Mamlaka ya Ngorongoro ili ikipendeza Wamasai wahamishwe ili kuiacha mamlaka ya ngorongoro iendelee kubaki kama urithi wa Taifa.
 
Tumehamia kwa Wamasai baada ya Wamachinga...
 
Kwa hiyo unaamini katika kutetewa? Huwezi kujitetea? Kama wewe huwezi kujitetea, ni wewe. Wengine wanaweza bila kutegemea hizo NGOs.
 
Kitenge ni nani? Kuna watu wenye akili na elimu waliokwisha kuandika mengi kuhusu hili suala na siyo huyo Kitenge kanjanja anayechumia tumbo lake bila haya.
Kina nani hao wenye akili na elimu ambao hayo maandiko yao mengi waliyoyaandika yalikubaliana na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika kreta?
 
Kina nani hao wenye akili na elimu ambao hayo maandiko yao mengi waliyoyaandika yalikubaliana na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika kreta?
Wewe umewekeza akili yako kuwa uharibu wa mazingira unasababishwa na wamasai tu. Ndiyo maana nikasema ingefaa zaidi mkasoma hizo research zilizofanyika na siyo nyie mnaozungumza kama kasuku tu kama alivyo huyo Kitenge mwenye uwezo wa kuzungumza maneno kama amemeza tape recorder bila kutumia akili.
 
Kwa hiyo population yenu ikifika 2million muachwe tu muishi Ngorongoro ?
 
Nadhani tatizo kubwa ni ongezeko ambalo linapunguza nafasi za kukaa. Jinsi watu wanavyoongezeka na pia mifugo kuongezeka basi wanyama pori wanaanza kupotea. Kama serkali ina mahali pa kuwapeleka wafugaji na mifugo yao nadhani itakuwa vizuri. Inatakiwa ikubukwe kuwa hadi sasa wamasai ni watu wanaofaidi sheria ya TZ wa ardhi kuwa ya umma. Sasa hivi wamasai wengi wametapakaa TZ nzima. Huko wanakokwenda ni TZ na hawabughudhiwi, lakini wao kudai kuwa hapo ni kwao toka enzi wanasahau kuna uwezekano wa wao kupewa sehemu. Kwa nini wanakataa kuhama, kama kuna sehemu mbadala. Mbona WaTZ wengine huhama kupisha ujenzi wa shule, viwanja vya ndege, n.k.? Kwani hao wanaohama hawakuwa na haki na sehemu hizo!!!
 
Wewe jiulize nani yupo nyuma ya Kitenge na Balile?
Kwanini Fred Manongi anatumia fedha za mkopo wa Covid kuwalipa watu waeneze chuki dhidi ya Wamaasai?
Manongi must go. Manongi ajiuzulu au afukuzwe kazi.
 
Na wengi mnaoshadadia kudhalilishwa na kutweza kwa utu wa Wamaasai ni viajiriwa vya NCAA. Vinapenda mshahara tu badala ya kwenda kwao kulima tangawizi na kufuga kuku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…