Mgogoro NCCR Mageuzi: Timu Mbatia wachukua ofisi, wasema umefanyika uhaini ndani ya chama, Mbatia bado ni mwenyekiti

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NCCR-Mageuzi, Edward Simbeye amezungumza na waandishi wa habari leo Mei 21, 2022 na kudai kuwa kilichofanywa na kundi lililojipa sura ya Halmashauri Kuu ndani ya chama hicho mapema leo ni uhaini.

Awali ilitolewa taarifa kuwa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia na Makamu Mwenyekiti Bara, Angelina Mtahiwa kutojihusisha na shughuli zozote za chama hadi Mkutano Mkuu utakapoitishwa ili wajieleze kuhusiana na tuhuma inazowakubali.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mwenyekiti wa azimio hilo, Joseph Selasini alisema pamoja na kusimamishwa kwa viongozi hao pia wamelivunja Baraza la Wadhamini la NCCR na kuteua wajumbe wapya ambao watasajiliwa kwa mujibu wa taratibu zitakazowekwa.

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza naye alikiri kupokea barua kutoka NCCR-Mageuzi kuwa kuna mabadiliko ya wajumbe wa bodi ya wadhami.

Baada ya tamko hilo ndipo muda mfupi baadaye Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Martha Chiomba, alifunga ofisi za chama hicho zilizopo Ilala, Dar es Salaam, ili kumzuia James Mbatia.

Baada ya tukio hilo, wanachama wanaomuunga mkono Mbatia ndani ya chama hicho walifika ofisini hapo na kufanikiwa kuingia ndani kisha kuzungumza na Wanahabari wakisema waliotangaza kumsimamisha Mbatia hawana mamlaka n ahata akidi haikutimia.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NCCR-Mageuzi, Edward Simbeye amesema:

“Kilichofanyika ni uhaini na uhuni ndani ya chama na hatuwezi kukubali kilichofanyika, chama kitakaa na kufanya maamuzi, kinachotusikitisha zaidi Msajili wa Vyama vya Siasa ameshiriki katika uhuni huu.

“Huwezi kuvunja Bodi ya Wadhamini au kumsimamisha Mwenyekiti kihuni.

“Msajili haoni hata haya, alijulishwa aliyekuwa Katibu Mkuu amesimamishwa inakuaje anapokea maamuzi yanayofanywa na watu kama hao.

“Sisty Nyahoza ndiye anaendesha haya makundi, anafadhili haya makundi na tuna uhakika, ukifika wakati tutaweka ushahidi hadharani. Huyu ndiye mhuni wa kwanza katika huu mchezo mchezo mchafu.

“Huyo aliyeitwa Katibu Mkuu (Martha Chiomba) alisimamishwa katika Kikao cha Kamati Kuu, anayekaimu ni Anthony Kom hakushiriki kwenye hicho kikao na hajui kama kuna hicho kikao walichofanya.

“Hao Wahuni walikuja kujaribu kufunga ofisi lakini tumewadhibiti na ndio maana tupo ofisini hapa, ofisi ipo chini ya wanachama. Tutaudhibiti uhuni wao, tumejipanga na tupo imara, hakuna ambaye ataweza kuivuruga NCCR Mageuzi.”


Pia Soma > NCCR Mageuzi yamsimamisha James Mbatia kufanya shughuli za Chama
 
Conglatultion for such a rescue
 
Wenyeviti wa hizi SACCOS kutoka Kaskazini wameona kama uenyekiti ni haki zao,Mbatia pamoja na Mbowe ni wenyeviti kwa muda mrefu hawana tofauti na raisi wa Uganda M7, hawa hawa ndio wanatoa mapovu majukwaani kudai demokrasia na katiba mpya wakati kwenye vyama vyao hakuna demokrasia wala mabadiliko ya katiba,ninachojiuliza wanang'ania uongozi kwa maslahi yapi? sio bure haiwezekani mtu miaka 20 baado upo palepale sijui wakipewa uraisi si ndio watajimilikisha nchi, wachaga acheni hizo bana, kuna maisha nje ya siasa na uenyekiti.
 
Hao Wahuni walikuja kujaribu kufunga ofisi lakini tumewadhibiti na ndio maana tupo ofisini hapa, ofisi ipo chini ya wanachama. Tutaudhibiti uhuni wao, tumejipanga na tupo imara, hakuna ambaye ataweza kuivuruga NCCR Mageuzi.”

A bit too late ...!
 
Kutakuwa kuna ujambazi umefanyika kuvamia na kuvunja NCCR hapo , Ujambazi huo ni mwendelezo wa ule wa wanawake 19 ndani ya CHADEMA. kughushi nyaraka za chama na saini za viongozi kisha kututwaa ubunge dezo .

Jambo hili liliwahi kufanyika pia kwa Diwani na Meya wa Wilaya ya Ubungo. Mh Boniface Jacob kuvuliwa umeya na udiwani na wahuni wa mtaani kwa kumwandikia barua mkurugenzi wa Manispaa hiyo .

Na mkurugenzi huyo aliridhia Ujambazi huo na kumpora uongozi Diwani na Meya wa wananchi wa kata na manspaa ya Ubungo.

Hayamabo hayakubaliki wananchi tuwe makini na mapichapicha kama hayo.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Mbatia alifurahia wakati ule selasini anawananga Chadema huku akilindwa na spika ****** . acha na yeye akipate pate cha mtema kuni kutoka kwa mchaga mwenzie Selasini .
"Wema huwa hauna gharama mahususi , Ila pindi unapoutenda ubaya jua ubaya huo utarudi" by dizata vina .
 
Tayari ishakuwa movie hii. Tumemaliza ya roho tuha sasa tunakinukisha chamani🔥👌
 
Sisty nyahoza hii ndio.michezo yake

Kaishindwa chadema

Sasa anahamia NCCR MAGEUZI

CUF walifanikiwa kuivunja vunja vipande wanailia timing chadema mdogo mdogo n mwenyekiti anaonekana atajaa TU hiz safar za ikulu hiz asidhan wanachama wanafurahia maana hazina majibu tunayotaka

MUDA N MWL MZURI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…