Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Ikumbukwe kuwa nchi huendeshwa kwa kodi. Bila kulipa kodi hakuna maendeleo na huduma za jamii. Pia, ili biashara iweze kukua sharti ilipe kodi kulingana na ukubwa wake. Iwapo utalipa kodi kubwa kuliko kipato chake, biashara hiyo itakufa.
Sio rahisi duniani kukuta nchi haitozi tozo au kodi kabisa, kwa sababu mapato yatokanayo na tozo na kodi yanasaidi kutunisha bajeti ya nchi inayoshughulikia huduma mbalimbali na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo miradi.
Hoja inakuja ni tozo ama kodi ngapi zinawekwa, unaziweka maeneo gani na viwango gani vya gharama za hizo kodi ama tozo unakata?
Pengine maswali haya ndiyo yanaleta mjadala mkubwa kwa nchi hasa zenye uchumi wa mdogo kama za kiafrika. Nchi hizi ni lazima zitumie kodi na tozo kupata mapato ya kujiendesha na kuhudumia wananchi wake kutokana na viwango vya uchumi ilivyonavyo.
Kwa mantiki hiyo hiyo, nchi zinatambulisha kodi na tozo mbalimbali za msingi ilikufikia malengo yake ya utoaji wa huduma kwa wananchi na kuleta maendeleo.
Kodi kwenye mapato kwa wafanyabiashara binafsi (income tax), kodi ya mapato kwa makampuni (corporate tax), kodi ya mapato kwa wafanyakazi (mfano PAYEE), michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii (Social security), Kodi ya majengo (property tax), kodi ya ardhi, kodi na ushuru wa kusafirisha na kuingiza bidhaa nchini, kodi ya ongezeko la thamani (VAT) , kodi ya faida ya mtaji (capital gains tax) na kodi nyinginezo nyingi.
Zipo kodi, ushuru na tozo lukuki tu kulingana na utafiti, maoni na rasilimali za nchi husika huwekwa kwa lengo hilo hilo la kukusanya mapato..
Mapendekezo
Watunga Sera
1. Utaratibu wa kodi nchini unapaswa kupitiwa kwa kuzingatia kanuni na madhumuni ya kodi,
ufaafu wa sheria zilizopo za kodi na uhalisia uliopo na hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kuwa
kila mlipa kodi mwenye sifa nchini anafuata masharti ya kodi.
2. Kuna haja ya kuwa na sera ya taifa ya kodi ambayo inazingatia mawazo ya walipa kodi na uwezo
wao wa kulipa kodi ili kubadili sera iliyopo ambayo inazingatia mahitaji ya matumizi ya serikali.
3. Mchakato wa bajeti unapaswa kuwa wa wazi na jumuishi. Mijadala na midahalo ya Umma kuhusu
kodi inapaswa kuhimizwa na kuwezeshwa.
4. Kuongeza kiwango cha chini cha mapato kwa mwaka ili kusajiliwa katika VAT kutoka Tsh milioni
100 kwa mwaka ili kuziondoa biashara nyingi ndogondogo na za kati kwenye kodi hii.
5. Kupunguza kiwango cha sasa cha VAT cha 18% kinachotumika kwa vyakula na vifaa vya
nyumbani hadi 14% kama ilivyo kwenye nchi nyingi za Kiafrika.
6. Kuandaa sheria rahisi ya kodi kwa ajili ya biashara ndogondogo na za kati na vyombo vingine,
mbali na Sheria ya Kodi ya Mapato. Sheria hii inapaswa kuandikwa kwa Kiswahili. Lengo liwe
kuhakikisha kuwa zinarahisisha taratibu za kujikadiria na kulipa kodi kwa kampuni ndogo na watu
binafsi.
7. Kupunguza idadi ya kodi na malipo ya mara kwa mara yanayotakiwa na serikali kuu na serikali za
mitaa na wakala wao.
8. Kuondoa kodi ya makadirio kwa biashara mpya
Wasimamizi wa Kodi
1. Kuchapisha kijarida cha kodi kilicho rahisi kueleweka kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili kila
mwaka kilicho na mabadiliko yote ya sheria ya kodi yaliyofanyika kupitia Sheria za Fedha kwa
mwaka, maagizo ya wizara na matangazo ya serikali. Mabadiliko hayo yanapaswa kuwa machache
ili zisiwachanganye watu.
2. Kuimarisha uwezo wa mamlaka ya usimamizi wa mapato kuchukua takwimu kwa usahihi, kutafsiri
kwa namna moja sheria za kodi, kuepuka kutoa makadirio kiholela na makubwa, na kupunguza
makosa ya kimaadili.
3. Kuboresha mfumo wa usuluhishi wa migogoro ya kodi kwa kufanya yafuatayo:
a. Kuanzisha kitengo huru ndani ya TRA kitakachofanya mapitio ya kiutawala ya pingamizi za
makario ya kodi kutoka kwa walipa kodi, kitengo ambacho ni tofauti na idara ya makadirio ya
kodi.
b. Kuondoa masharti ya kulipa 1/3 ya kodi kama sharti la kupokea pingamizi la mlipa kodi kwa
ajili ya kupitiwa.
c. Kuboresha upatikanaji wa huduma za Bodi ya Rufaa za Mapato ya Kodi kwa walipa kodi wa
mikoani kwa kufungua masjala mikoani.
d. Kuanzisha utaratibu huru wa kupitia migogoro kabla ya mahakamani sawa na mradi wa
majaribio wa TAS.
4. TRA wanunue EFD mashine na kuwapa (au kuwakopesha) wafanyabiashara kwa sababu ni chombo chao cha kukusanya kodi
Walipa Kodi
1. Wachukulie kitendo cha kulipa kodi kama ni uzalendo
2.Watunze kumbukumbu Ili kujua kuwa biashara husika ina faida au hasara sharti kuwapo ukokotoaji wa mapato na matumizi
3. Watoe risiti(EFD) kwa kila bidhaa wanayouza
Serikali Kuu
1. Kupunguza matumizi yasiyo natija kwenye shughuli zake hususan ununuzi wa magari kama Landcruiser V8. Yatumike magari yenye ukubwa mdogo wa injini ili kugunguza gharama za uendeshaji
2. Kusitisha safari zisizo za lazima ndani na nje ya nchi
3. Kuhakikisha kuwa mipango iliyopo kwenye mpango kazi wa Taifa ndiyo inatekelezwa
4. Kuwachukulia hatua wafanyakazi wa serikali wanaokutwa na hatia kwenye ripoti ya CAG
====
Pia soma: Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024