The Genius
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 822
- 2,095
Baada ya Mgogoro mkubwa wa Kanisa uliozaa Makanisa mawili - Western Roman Catholic Church na Eastern Orthodox Catholic Church mwaka 1054, Kanisa la Magharibi ambalo ni Western Roman Catholic Church liliendelea kuandamwa na migogoro na migawanyiko tofauti na Eastern Orthodox Catholic Church ambalo halijawahi kukumbwa na migogoro mikubwa au hata migawanyiko.
Mgogoro wa kwanza mkubwa kutokea ndani ya Western Roman Catholic Church ulianza Mwaka 1303. Papa Boniface VIII alimkemea Mfalme wa Ufaransa kwa kuwatoza Kodi Wachungaji (the clergy). Mfalme alijitetea kuwa alikuwa amepata ushauri wa Bunge kufanya hayo. Kadhalika, Papa alikuwa ameshambuliwa na Bunge la Uingereza lililokuwa linampinga kwa kumuingilia Mfalme Edward I wa Uingereza.
Hata hivyo, Mfalme wa Ufaransa alimtendea ukatili Papa Boniface VIII ambaye sasa alikuwa ni mzee na kumsababishia mauti Mwaka 1303. Papa mpya alitoa tamko (a Bull) akilaani ukatili aliofanyiwa Papa aliyekuwa mtangulizi wake. Lakini naye Papa mpya aliweza kuishi wiki 4 tu baada ya kutoa tamko lile.
Kwa kipindi cha mwaka mzima, hakukuwa na Papa aliyechaguliwa. Ndipo akachaguliwa Papa Clement V. Huyu hakuwa Mtaliano kama ilivyokuwa desturi, bali alikuwa ni Mfaransa. Yeye aliwateua na kuwatangaza Makadinali wapya 12 wote wakiwa Wafaransa isipokuwa mmoja aliyekuwa Mwingireza na hii ilikuwa ni kutaka kupoza uadui uliokuwepo baina ya Ufaransa na Uingereza.
Papa Clement V aliamua kuhamisha Kiti cha Papa au Makao Makuu ya Kanisa kutoka Rumi na kupeleka Avignon katika Jimbo la Provence nchini Ufaransa. Upapa huo ambao ulijulikana kama Upapa wa Avignon (The Avignon Papacy) ulidumu kwa kipindi cha muda wa miaka 70. Watu wengi walipinga kitendo cha kuhamisha Kiti cha Papa kilichoambatana na mapapa 7 mfululizo kuchaguliwa kutoka miongoni mwa Wafaransa.
Wakati huo, Vita vya Miaka 100 baina ya Ufaransa na Uingereza vilikuwa vimeanza. Hili lilizidisha Waingereza kuchukia mamlaka ya Papa kutokana na ukweli kuwa muda wa miaka 70, Kiti cha Papa kilikuwa kinashikiliwa na Wafaransa ambao walikiwa ni adui wakubwa wa Uingereza. Hata hivyo, kuhamishia Kiti cha Papa nchini Ufaransa kulimaanisha gharama kubwa kwa Makanisa ya Ufaransa pia.
Mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Papa katika kipindi hicho alikuwa Mtakatifu Catherine wa Sienna ambaye alikuwa Mtaliano. Aliwahi kumueleza Papa Gregory XI bila kupepesa macho akisema: "Kama ungeliweza kufungua macho ya akili zako, Baba Mtakatifu kuwa ni bora zaidi kuokoa roho kuliko kung'ang'ania kupata utajiri wako"!
Papa Urban V (1362 - 1370) alifikiria kurudisha Kiti cha Papa mjini Rumi. Baada ya kutembelea Rumi alikuta majengo yamechakaa, akaona vigumu kuachana na anasa za Avignon. Papa Gregory XI (1370) alifanya maamuzi magumu na kukirudisha Kiti cha Papa tena Rumi, lakini alifariki mwaka uliofuata.
Makadinali ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa ni Wafaransa waligawanyika na katika mioyo yao walitaka Kiti cha Papa kiendelee kubakia Ufaransa. Hata hivyo, uchaguzi wa Papa mpya ulitakiwa sasa ufanyikie Rumi. Kule Rumi kulikuwa na umati wa watu waliokuwa wanaandama wakipiga kelele wakisema: "Sasa ni zamu ya Papa kutoka Rumi"! Papa aliyechaguliwa hakuwa Mrumi, wakamauita mtu wa kutoka Naples kuwa Papa Urban VI. Huyu hakutaka mjadala wa kurudisha Kiti cha Papa kule Avignon.
Papa Urban VI alitengeneza maadui wengi miongoni mwa Makadinali kutokana na msimamo wake wa kukataa kurudisha Kiti cha Papa kule Avignon. Wakaitisha mkutano ili kutangaza kuwa hakuwa Papa hal ofali kwa kuwa alikuwa amechaguliwa kutokana na shinikizo la watu.
Makadinali wa Ufaransa kwa kuwa walikuwa na wingi wa kura wakamchagua Mfaransa mwenzao na kuwa Papa Clement VII. Huyu alikuwa ni Askari na aliyekuwa rafiki wa Mfalme wa Ufaransa hivyo akahamia Avignon.
Papa Urban VI akatangaza kuwa mchakato mzima wa kumchagua Papa Clement VII ulikuwa batilo na hivyo akakataa kumtambua. Papa Clement VII akateua Makadinali wapya kubadili nafasi za wale waliohamia Avignon. Huo ndio ukawa mwanzo wa mgawanyiko au schism (1378 - 1417). Hivyo kulikuwa na Papa wawili kwa kipindi cha miaka 39. Papa wa Rumi alitambulia na Italia, Uingereza, Ujerumani, Scandinavia na Ureno. Papa wa Avignon alitambuliwa na Ufaransa, Scotland na sehemu ya Ujerumani.
Mgogoro huo ulifikishwa katika Chuo Kikuu, Paris kwa ajili ya utatuzi. Wasomi wawili wa Chuo Kikuu, Paris waliotoa muafaka ni Pierre (Peter) d'Ailly (1350 - 1420) na Jean (John) de Gerson (1363 - 1429). Kipindi hiki ndio ulikuwa mwanzo pia wa Kanisa la Moravian kumeguka kutoka Western Roman Catholic Church.