Grand Canyon
JF-Expert Member
- Jan 2, 2020
- 545
- 1,191
Jina Palestina linatokana na neno la Kilatini Palaestina na neno la Kigiriki Palaeistine. Maneno haya mawili yanatokana na neno la Kiebrania Pelesheth. Biblia inatumia neno Pelesheth linatafsiriwa Filistia kwa Kiswahili kwenye Biblia.
Linarejelea eneo la Pwani ya Mediterenia lililokaliwa na Wafilisti.
Katika Biblia majina Palestina, Kanaani, Israeli, Nchi ya Ahadi yana maana moja. Wayahudi walipotoka Misri Mungu aliwaahidi kuwapa Kanaani waimiliki. Wakati huo ilikuwa ikikaliwa na Wafilisti. Abrahamu, Isaka na Yakobo waliishi Kanaani/Palestina kabla ya Yakobo kuhamia Misri.
Waliporudi waliwatimua Wafilisti nao wakaimiliki nchi ya Kanaani/Palestina. Mwaka 1070 BC Daudi akafanya Yerusalemu kuwa mji wake mkuu. Sulemani akamjengea Mungu hekalu Yerusalemu.
Mwaka wa 70 AD Roman Empire iliteketeza Yerusalemu na hekalu lake na kuwapeleka Wayahudi uhamishoni katika maeneo mbali mbali ya milki hiyo.
AD 130 Emperor Adrian alilijenga upya Yerusalemu na kuliita Aelia Capitolina. Akawapiga marufuku Wayahudi kukanyaga katika jiji hilo kwa miaka 200. Kisha Mama ya Emperor Constantine aliyeitwa Hellen alitembelea Yerusalemu na akaanza kujenga maeneo matakatifu (Shrines) na Makanisa.
Katika karne ya 7 AD waislamu waliteka jiji la Yerusalemu na Caliph Abd al-Malik ibn Marwan akajenga Msikiti wa el Aqsa. Waarabu walihamia Palestina kipindi hiki hasa kuanzia mwaka wa 638 AD.
Baada ya Adolf Hitler kuwaua Wayahudi karibu milioni 6, Uingereza iliamua kuwarudisha kwao yaani Israeli/Kanaani/Palestina. Hivyo mgogoro ukazuka.
NB😛alestina ni Geographic location. Kuna wapalestina waarabu, Wapalestina Wayahudi, nk. Hata mimi nikipata uraia nitaitwa Mpalestina mwenye asili ya Tanzania.
MFANO: Tuseme ni mwaka 1967. Serikali inaanzisha vijiji vya Ujamaa. Watu wa Kijiji A wanapelekwa Kijiji B ambacho kina huduma zote za kijamii. Baada ya wanakijiji kuondoka watu wengine wanahamia Kijiji A. Wanajenga na kulima mashamba. Kisha mwaka 1985 sera ya ujamaa inakufa. Watu waliohamishwa wanarudi Kijiji A wanakuta tayari watu wengine wameshajenga na kuishi hapo. Mzozo unazuka. Nani atatatua mzozo huu?
Hiyo ndiyo hali ya Palestina. Wayahudi waliondoshwa mwaka 70 AD, Waarabu wakahamia 638 AD. Wayahudi wakarudi nyumbani 1947 AD. Waarabu wanawaona Wayahudi kuwa wavamizi, na Wayahudi wanawaona Waarabu kuwa wavamizi.