"Mwalimu, post: 21757350, member: 11689"]
Unafikiri athari za mgogoro huu zitakuwa kubwa kiasi gani kwa pande zote mbili hususan Qatar itaathirika vipi kwa kufungiwa milango na Saudia?
Mkuu
Mwalimu mgogoro unahusu pande mbili zenye mafuta kwa wingi duniani.
Kwa Saudia kwasababu wana 'black gold'' haitegemewi kuathirika
Qatar itaathirika hasa ikizingatiwa kuwa chakula na huduma nyingine zinatoka Saudia
Kumbuka Saudia ni Taifa kubwa sana ukilinganisha na Qatar
Mgogoro ulianza kwa panic ya watu kukusanya vyakula na huduma zingine ambazo Qatar wanategemea nchi ya Saudia. Ndiyo maana baada tu ya mgogoro, Turkey na Iran zili 'rush' kutoa msaada wa chakula ili isiwe ''bargaining chip'' itakayowalazimisha kukaa mezani
Qatar ina shirika kubwa la ndege ambalo linatumika kama 'Hub' ya kuingilia middle east
Shirika hilo linaendeshwa kisasa na linatoa huduma kwa kiwango cha kimataifa haswa
Kufunga mpaka kutaathiri sana shirika, kwani mahujaji wa Mecca katika Hajj na wale wanaokwenda kuzuru 'umra' itababidi watafute mbadala ambao ni Gulfu air au Emirates
Hilo litatoa mwanya kwa mashirika hayo ya UAE kujitanua na shirika lao kuvia
Tatizo lingine ni Television ya Aljazeera ambayo ni maarufu sana middle east and far
Umaarufu wake ni katika kueleza yale yasiyojulikana katika falme za kiarabu
Kwa mtazamo huo, ima Aljazeera itaathirika kwa kulazimishwa kufungwa kama madai ya kurudisha uhusiano, au Aljazeera itaendelea kuanika habari nyeti za mashariki ya kati
Ni aljazeera pekee ndiyo inaeleza migogoro ya ndani ya Arab World kwa kina na uchunguzi ikigusa falme ya Saudia Arabia na Israel kwa undani wake
Kwa upande wa nje, Qatar italazimika kusitisha misaada kwa maeneo kama Gaza ambako wamejihusisha na ujenzi baada ya kubomolewa na Israel miaka michache iliyopita
Raia wengi wa Qatar wanaishi nchi za Uarabuni kama Saudia watalazimika kuondoka
Mahusiano ya kueloeana na taratibu za uhamiaji zitawaathiri wahamiaji kutoka Qatar
Qatar inataraji ku host FIFA 2022 na hilo litakuwa na athari.
Kuna uwezekano vikwazo vikiendelea FIFA ikafikiri upya kuhusu ushiriki wake
Kwahiyo Qatar inasimama ku lose kuliko washirika wa GCC au Aarab world in general
Swali, je watahimili vikwazo walivyowekewa?
Huoni kwamba kwa kuitenga Qatar inaweza kuchochea wao kusogea zaidi upande wa Iran? Juzi tu hapa tumeona Iran ikisafirisha shehena ya misaada kwenda Qatar.
Yes Qatar ni mshirika wa Iran ambaye ni mshirika wa Russia.
Baada ya uhusiano wa Saudia na US kulega lega (Obama) Saudia iliwageukia Russia.
Saudia haiamini Russia kutokana na ukaribu wake na Iran.Russia ni rafiki wa adui
Kwa kuona hilo, Saudia wakaamua kumpa Trump mapokezi makubwa na mbadala wake ukawa kuuziwa silaha kwa mabilioni ya dola, yaani wakiondoka Russia na kurudi US
Hilo limechagiza Iran kuingia kati na kuisadia Qatar kwa chakula ikishirikiana na Turkey
Wakati huo huo Turkey inaona kama haitaingizwa EU basi itageukia Iran.
Kumbuka Turkey ni mwanachama wa NATO na hivyo US inamwangalia kwa jicho la karibu
Uhusiano wa US na Turkey ni muhimu kwa Europe na Israel
Kumsogeza Iran kwa ukaribu na Turkey kunafanya equation kuwa complicated (Complicated)
Na hapo tusisahau kwamba Marekani ana kambi kubwa ya kijeshi nchini Qatar. Kwa kitendo cha Marekani kuonekana akiegemea zaidi upande wa Saudia inaweza kuathiri mahusiano yake na Qatar na inaweza kuleta sintofahamu juu ya uwepo wa majeshi yake Qatar
Ndiyo US wana base Qatar wana air base Kuwait.
Kwa kutambua nature ya mzozo na jinsi unavyoweza kuathiri nchi hiyo, US wamemuomba (nyuma ya pazia) Kuwait awe msuluhishi wa mzozo wa Qatar
Hili litaisumbua sana US kwasababu ni upanga unaokata sehemu mbili (double sword)
Kumwacha Qatar ni kuruhusu influence ya Iran na Russia kusambaa middle east
Kumhodhi Qatar ni kuwakimbiza washirika kama Saudia ambao ni chimbuko la ''magaidi''
Kwa kitendo hicho, US wata play safe, bila kuathiri mahusiano na nchi za Uarabuni dhidi ya Qatar na bila kutoa mwanya kwa Qatar kuangukia Iran-Russia kikamilifu