Moja ya ahadi za kampeni za Trump ilikuwa ni kupunguza / kuachana na biashara ya kujihangaisha na masuala ya mataifa mengine ("America First"). Verdict: Hakuwezi kuwa na boots on ground Saudia kutoka Marekani kutokana na suala hili tu, kama Trump atataka kuwapendeza wapiga kura wake.
Mkuu
Mlenge , sera ya America first ni Rais Trump kuwa 'ill informed' kwa mambo ya dunia na hata ya nyumbani
America first haiwezi kuzidi masilahi mapana ya nchi hiyo ambayo ni kutawala Dunia
Trump alipouza sera ya America First, ilipokewa na wanaoamini kuwa bila kujiingiza katika masuala ya kimataifa , Wamarekani watakuwa na maisha mazuri.
Kwa mfano, Trump alisema US inatoa misaada inayoweza kutumika kuimarisha maisha ya watu.
Takwimu zinaooonyesha misaada ni chini ya a(2%?) tena ikiwa na return katika security ya US
Majeshi ya US kule Ujerumani si kuilinda nchi hiyo, ile ni ''strategic point'' ya usalama wa US.
Majeshi ya US Korea Kusini si kuilinda Korea, ni kwa US kwa kuangalia China na North Korea. South Korea ina askari 30,000. Trump hawezi kuyaondoa , aliposema hakujua 'ill informed'
Majeshi ya US kule Japan ni kwa ajili ya US. Mgogoro wa kisiwa cha South China na kujitanua kwa China kunalazimu US wawe karibu. Trump hakujua kwa ''ignorance''
Hadi sasa, kuna majeshi ya US kule Saudi Arabia kwa masilahi yake.
US wanasaidia Saudia vita ya Yemeni na Syria katika logistic zote.Kuna boot tayari Saudia
Saudia ikiwa na holy sites, US haiwezi kuingilia kama inavyofanya kwa vinchi vingine. Huwezi kuona boot hadharani, boot zinakuwepo kwa strategy
Kutibuana na Saudia ni kuzua mtafaruku na Islam world, na hilo litawaunganisha Sunni, Shia, Ismailia. Mkakati wa divide and rule utakwama, masilahi ya US yatakuwa hatarini ikiwemo Israel
Suala la Khashoggi US inatafuta njia muafaka kukabiliana nalo, Trump ana hangaika. Vinginevyo, hilo kama halimhusu kwa America first, mbona linamsumbua sana!
Mkuu America first inaeleweka kwa wapiga kura wake wanaoamini kuzuia immigrants kutawapa kazi na si kwenda shule.
Kuna kazi milioni 7 hazina watu, bado watu wake wanaamini mtu anayeokota machungwa ni tatizo kwa US. Midterms imeonyesha jinsi wasomi na independents wanavyomkimbia Trump
Mwaka 2017 America first haikujali APEC, wanaona China inavyojitanua wanarudi kwa kasi.
America first iimefanya nchi hiyo kuanza kutengwa na kupoteza Influence katika world stage.
Kilichotokea Paris wakati wa Armistice kinaeleza kitu
CIA wanapotoa taarifa ''leak' kuhusu MBS na mauaji wanafanya makusudia ili Trump asiweze kulifukia.Wamebaini anataka kufanya hivyo kwa masilahi yake na familia na si America
Suala sasa lipo Congress. Intel community zinajua jamaa ni ignorant na ill informed, haziwezi kuwa katika kundi la Trump. Zinajua America first kwa maana halisi si maana ya Trump