Peter Madukwa
JF-Expert Member
- Sep 20, 2012
- 3,139
- 2,488
Habari ndugu wana JF
Kama inavyoonekana katika vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mgogoro kati ya Urusi na Ukraine.
Mgogoro huu chanzo chake kikubwa ni dhamira ya UKRAINE Kujiunga na Mkataba wa NATO ambao pia unahusisha MAREKANI.
Kwa mujibu wa madai ya Urusi wanasema kuwa hawapendezwi kuona Ukraine inajiunga na NATO kwa sababu wana hofu ya usalama wa mipaka yake ambapo endapo UKRAINE ikijiunga na NATO basi Urusi wanaamini kuwa MAREKANI itaweka millitary base UKRAINE ambayo ipo mpakani na URUSI na hivyo kwa maelezo ya Rais Viladmir Putin wa Urusi ni kuwa kiusalama itakuwa hatari zaidi ktk nchi yake jasa ukizingatia nchi hizi ni mahasimu ktk masuala ya kijeshi na uchumi kwa kuwa zote zina nguvu kubwa ya kiuchumi (RUSSIA VS USA).
Kwa sasa hivi imekuwa siyo mgogoro tena ambapo imeripotiwa mapema leo asubuhi majeshi ya URUSI yamezingira karibu eneo lote la mipaka ya UKRAINE kupitia nchi jirani ikiwemo Belarus.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari tayari Urusi imeaanza mashambulizi dhdi ya Ukraine na hivyo kusababisha madhara ya vifo vya watu 6 huku wananchi wengi wa UKRAINE wakionekana kukimbia nchi kuelekea nchi za jirani.
Mapema leo Rais wa Urusi amewataka wanajeshi wa Ukraine kusalimu amri na kuweka silaha chini kabla hawajasambaratishwa huku akitamba kuwa nchi yoyote itakayojaribu kuingilia mgogoro huo atakiona cha mtema kuni.
Hapa nchini kwetu ukiingia ktk mitandao watu wengi wanaaonekana kuleta ushabiki wa kivita.. wapo ambao wapo upande wa Urusi na wapo ambao wapo upande wa Ukraine wakiamini kuwa NATO hasa marekani inaweza kuingilia vita hiyo ili wazichape na Urusi.
Kimsingi ndugu zangu watanzania VITA siyo jambo la kushabikia; ktk ulimwengu wa sasa ambao uchumi ni wa kutegemeana ukiacha athari ya moja kwa moja kama vile mauaji ya raia wasio na hatia, uharibifu wa miundombinu ktk eneo la vita lakini VITA huleta athari ya uchumi wa dunia ikiwemo mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu kama mafuta ya petrol na diesel ambayo kupanda kwake huleta athari kubwa ktk uchumi wa dunia hasa ktk NCHI MASKINI/ZINAZOENDELEA ambapo uchumi wetu ni wa kusuasua.
Shime ndugu zangu vita siyo jambo la kushabikia badala yake tunatakiwa kuomba mgogoro huu uishe salama na kwa muda mfupi tuombe mashirika ya kimataifa ikiwemo UN watafute suluhu ya haraka ya vita hii kati ya UKRAINE na URUSI ili kunusuru athari zinazoweza kujitokeza.
Mapema leo Papa wa Kanisa Katoliki amesema kuwa siku ya Jumatano ya majivu ni siku maalum ya maombi kwa ajili ya kumwomba Mungu kumaliza mgogoro wa Ukraine na Urusi ili dunia iendelee kubaki kuwa sehemu salama ya kuishi
Mungi ibariki Tanzania, Mungu Ubariki ulimwengu kuwa sehemu ya amani badala ya vita.
Pichani: RAIA WA UKRAINE WAKIKIMBIA NCHI YAO BAADA YA URUSI KUANZA MASHAMBULIZI YA MABOVU.
Wanaoumia ni raia wasio na hatia
Updates: 1.3.2022
Bei ya mafuta imepanda ktk soko la dunia
Updates: Tarehe 5.4.2022
Bei ya mafuta ya petroli yazidi kupaa kufuatia kuadimika kwa bidhaa hiyo inayochangiwa na athari ya vita ya Ukraine na Russia ambao unakwenda sambamba na vita ya kiuchumi