lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Kinachoonekana baina ya Pro Russia dhidi ya Pro NATO/ USA/ Ukraine sio ushabiki Bali ni historia.
Histori inatuambia kulikua na Kambi tatu.
1) West ikiongizwa na USA UK na western wengine.
2) East ikiongizwa na USSR ambayo ndo Urusi East German na wengine.
3) NAM, kwa Kiswahili nchi zisizofungamana na upande wingine zikiongozwa na Yugoslavia na wengine Tanzania ikiwa ni mojawao.
Historia nyingine.
Kipindi Cha ukoloni,hasa kwa upande wa Afrika Nchi za East zikiongozwa na USSR zilitoa misaada ya silaha,mafunzo ya kijeshi,elimu,fedha,hifadhi,ushauri,na Kila aina ya motisha katika vikao vya umoja wa mataifa na hata umoja wa jumuiya ya madola kwa wapigania uhuru na nchi ambazo zilikua bado zinatwaliwa na wakoloni.
Historia inatueleza zaidi.
Nchi za west zilikua kinyume kabisa na harakati za ukombozi,
Nchi hizo zikiongozwa na USA na UK zilipinga nna yoyote ya kuwasaidia Viongozi ama nchi zilizokua zinadai haki zao za kujitawala.
Wakoloni hawakutaka kabisa kuziachia nchi za kiafrika na hata nchi nyingine zilizokua zikidai uhuru wao,ndipo wananchi wa nchi hizo wakaamua kudai haki zao kwa njia mbalimbali.
Baadhi ya njia hizo ni matumizi ya nguvu kwa kutumia silaha,na njia nyingine ni kuiomba jumuiya ya kimataifa kuziwekea vikwazo nchi wakoloni,mojawapo ya nchi wakoloni zulizosumbua sana na ilihitajika kuingia vita nao vya msituni ama vya mtaa kwa mtaa ni Makaburu wa Afrika kisini na wareno wa msumbijina watwala wa Angola.
Nchi za west ambazo kwa ujumla wake ndio hizi za NATO iliyokuwepo kabla ya kuvunjika kwa USSR hazikutoa msaada wowote kwa wapigania uhuru,na kibaya zaidi zilipinga vikwazo,zilipinga matumizi ya nguvu na kwa kusikitisha zaidi zilizisaidia nchi wakandamizaji kwa Hali na Mali.
Kwa mfano zilipinga Makaburu wasiwekewe vikwazo na wasipigwe vita.
Cha kushangaza baadhi ya wapigania uhuru hawakupewa heshima stahiki.kwa mfano mfungwa maarufu duniani,mpigania haki na mwanasiasa maarufu wa Afrika Bwana Nelson Mandela alipewa jina baya kabisa na USA .
Aliwekewa kwenye orodha namba moja( 1) katika orodha ya watu hatari zaidi duniani.
Kwa lugha rahisi Marekani ilimtangaza nelson Mandela kama mtu hatari kabisa duniani.
Walimweka namba moja na kufuatiwa na wahalifu wengine.
Kwa maana hiyo Mandela alionekana ni Gaidi.
USA ,UK,Israel na nchi nyingine ziliipa South Afrika ya Makaburu teknolojia ya nyukilia,hivyo ikawa na silaha za nyukilia ili nchi za Afrika zisiiguse.
Kumbuka nchi za Afrika zikiongozwa na Tanzania zilikua zinaendesha mafunzo ya kijeshi kwa wapigania uhuru.
Kwa hiyo kama Makaburu wangeona wanazidiwa wangeweza kuzipiga kwa nyukilia nchi watetezi wa Akina madela.Tanzania ikiwemo.
Watetezi wakubwa wa Makaburu walikua ni NATO.
Wasaidizi wakubwa wa wapigania uhuru walikua ni Urusi,china,Yugoslavia na nchi nyingi za East.
Kusema kweli majeshi ya Cuba yalifanya kazi iliyotukuka ya kuwadhibiti wanajeshi makatili kabisa wa Makaburu waliokua wakiwapa kipigo kikali sana wapigania uhuru wa Angola,Afrika kusini na msumbiji.
Makaburu walipewa mafunzo,silaha,na teknolojia na USA UK na hata Israel.
Inaendelea.
USA na NATO walivamia kwa sababu tofauti nchi za mashariki ya kati,
Kama Iraq,Syria na Libya.
Wameziwekea vikwazo nchi ya Iran,
Wameshiriki migogoro katika nchi za Lebanon,
Watu wanakumbuka machafuko yaliyokua yanafanyika nchi za south America mfano Nicaragua,Honduras chanzo ni USA,
Watu wanakumbuka Korean war,
Watu wanakumbuka Vietnam war,
Watu wanakumbuka Cambodian war.
Haya yote USA Alikua ana mkono wake direct ama indirect.
Hawaoneshi kushughulikia mgogoro wa Palestina na Israel kwa umuhimu mkubwa,na kutokujali kilio Cha wapalestina.
Kwa nchi za mashariki ya kati nchi zinazoonekana kujali na angalau kushughulikia migogoro ya waarabu na mashariki ya kati ni Urusi,na baadhi ya nchi za East.
Kwa machache hayo hiyo ndizo zinazoweza kuwa sababu ya watu ama nchi kushabikia operation hii ambaya inaonekana ni kama operation ya east dhidi ya west.
Hapa kinachoonekana ni kama watu wanafurahia Ukraine kupigwa.
Lakini ukweli ni watu wanaofurahia operation hii ni kuona majeshi ya NATO na Bosi wao USA wakidhibitiwa au wakiadhibiwa na Urusi.
Watu wanaoshabikia Urusi ni kwamba hawana tatizo na Ukraine,wao tatizo lao ni USA.
Wanafurahia kuona kuwa kumbe USA Kuna sehemu hafurukuti.
Wanafurahia kuona mwanafumzi wa USA anaadhibiwa mbele ya USA na USA hafanyi chochote.
Wanafurahia kuona mtesi wao anadhalilishwa na Kuna mtu anaweza kumfanyia chochote.
Ukraine anaadhibiwa kama ujumbe Kwa mwalimu wake.haya ni mambo machache ya kihistoria yanayofanya watu wakumbuke uonevu wa USA na NATO yake.
Wanafurahia kuona aliewatesa Sasa anateswa,hata kama ni indirect.
Kwa kumaliza,ni kwamba wanaoshabikia pro Russia ni kutokana na historia ya tabia za USA na NATO.
Kiisimamo na kimatendo dhidi ya nchi fulanifulani.
Hivyo wanaona kama Urusi amekuja kuwaaibisha na kuwadhalilisha.
Wanaona kama Urusi kaja kuwa komboa ama kuwa semea.
Watu hawaichukii Ukraine kabisa ,Bali wanamchukia "handler" wake.
Wanafurahia kupigwa Ukraine kwani wanaamini anapopigwa Ukraine "anaumia USA na NATO."
Kwamba anapopigwa Ukraine mfadhili anaaibika.
Hata mpigaji ni kama anapeleka ujumbe Kwa mwalimu.
Kinachowafurahisha pro Russia ni kuona USA inafedheheshwa kwa sababu Huwa inafedhehesha.
Operation hii imeamsha machungu na mitazamo ya kihistoria.
Ndio maana Viongozi wa Afrika hawakutilia maanani ombi la Zelensky la kutaka kuongea nao kwa sababu Zelensky ni rafiki wa watesi wa Afrika..
Tamati.