Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Huko Morogoro umetokea mgogoro kati ya wananchi na wamaasai, chanzo cha mgogoro ni wamaasai walipeleka ng'ombe wao mtoni kunywa maji.
Maji ya mto husika hutumiwa kwa matumizi ya kila siku majumbani na wakazi wa eneo hilo, ipo sheria inayokataza mifugo kupelekwa ndani ya mto kunywa maji ili kuzuia uharibifu wa mtiririko wa maji japo wamaasai hukaidi wanavijiji wanapowazuia.
Ukaidi wa wamaasai hutokana na wao kuruhusiwa kutembea na silaha za jadi ambazo huzitumia kuwadhuru wananchi, ila kwenye tukio hilo wananchi waliwazidi nguvu wamaasai na kuishia kuwakata mapanga ng'ombe.
Jeshi la polisi litumie busara ya usuruhishi kwenye jambo hilo japo wao wanauita ni uhalifu, hayo makundi mawili yanaishi eneo hilo na wanategemea mto huohuo, hivyo jeshi halinabudi kuwaelimisha wamaasai wafuate sheria za nchi kuhusu mazingira kwa kutopeleka ng'ombe ndani ya mto.