Wewe Magufuli akishinda atakutia njaa wewe na familia yako,badilika kijana.
Mimi 2015 nilimshabikia na kumpigia kura Magufuli nikitegemea atarudisha nidhamu kwenye utumishi wa umma ndiyo jambo lililokuwa linanikwaza kwenye utawala wa Kikwete kipindi hicho nikiwa mtumishi wa umma...
Mimi sijawahi kuwa mpenzi wa siasa, ni sijawahi kupiga kura kwa sababu moja
Niliona CCM wataendelea kufanya upuuzi ule ule na upinzani haujaweza nionyesha mtu wakusema huyu atatuvusha. Wengi midomo tu.
Ila mwaka huu, nampigia Magufuli. Nimeajiriwa miaka 10 kwenye sector binafsi ilikuwa inafanya tenda za serikali. Najua vizuri upuuzi wa serikali. Mpaka nilipoacha kazi na kujiajiri 2016.
Siwezi kuitetea CCM maana najua upuuzi wao ndio umetufanya tubaki masikini. Ila Magufuli, Ahh kura yangu anaipata. Ila asikae zaidi ya 2025.
Nafanya hivi nikijua kabisa, tutake tusitake mambo anayo yafanya Tanzania tuna yahitaji sana.
Tunahitaji kusimamia rasimali zetu ili tuache kutegemea kodi. Uchumi wetu ulikuwa wa ajabu sana.
Yaani mbane mfanyabiashara kodi, upate hela ya kumlipa mwalimu mshahara. Kama tunataka tutoke, lazima tuongeze vyanzo vingine vya mapato kama kuuza umeme nje, treni na bandari mizigo iongezeke. Hivyo vikiwepo, tuweze kupunguza mzigo kwenye kodi kwa wafanya biashara.
Mwache amalize hizi ujenzi, then kitaeleweka.