Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Mgombea uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Rosemary Linda ameomba kuwe na tume uhuru ya kuhesabu kura ili kuondoa dhana ya kuibiwa kura.
Rozimele ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, Septemba 24, 2022 mara baada ya kujitambulisha kama mgombea katika nafasi hiyo.
Amesema ili kuepuka udanganyifu unaoweza kujitokeza, lazima kuwepo na tume huru ya kuhesabu kura huku akiomba wanafunzi wa shule ya sekondari Sengerema ndiyo wateuliwe kuhesabu kura.
Kutokana na hofu hiyo, Katibu wa CCM, Wilaya ya Sengerema, Mhusini Zikatimu amesema hakuna kura itakayoibiwa na kura hizo zitahesabiwa hadhari.
CCM ipo katika chaguzi za Jumuiya zake za Vijana na wanawake ngazi ya wilaya.
Chanzo: Mwananchi