Quinine,
Hii ni moja ya blunders walizofanya Chadema Kagera wakati wa ku recruit wagombea. Si kwa Phocas tu bali wako na wagombea wengine katika mkoa huu ambao nina wasi wasi nao. Ni rahisi sana kununuliwa na wenye pesa sisi m.
Namfahamu kweli Phocas kama mwana harakati na mchukia uovu wa nchi hii na anaelewa vema taabu za nchi hii ingawa binafsi yeye anayo pesa nzuri ya kumsaidia kuendesha maisha yake. Nimewahi kuzungumza naye mara nyingi. Yeye tangu mwanzo hakuwa na mpango wala kusudi la kugombea mbali na kwamba alishawishiwa na wana sisi m wenyewe waliokuwa wamegalagazwa na yule mama wa sisi m mfanyakazi wa UWT anayejulikana kwa jina la Asumpta.
Inaelekea viongozi hao waliingia mkenge bila kufuatilia vizuri, wakamuondoa huyo Walter aliyekuwa amejitolea mwanzo kuingia vitani, badala yake wakamuweka huyu Bwana dakika za mwisho under the influence of these sisi m traitors. Haya ndio matokeo, tunayajutia na yametutia uchungu sana.
Well, tunsonga mbele. Tunahitaji kuijenga Chadema yenye nguvu huko Kagera. Najua kitu kimoja, siwezi kwenda sisi m kwa namna yoyote ile kama haijabadilika. Ni bora nikishindwa kabisa kuvumilia kukaa Chadema nitarudi kijiweni kuishi bila chama kama nilivyowahi kuwa huko nyuma, maana siamini kama kuna chama makini na cha hakika ingawa bado kichanga kama Chadema.