GE2025 Mgombea Mwenza NCCR-Mageuzi: Wakulima watapanga bei ya mazao yao bila kuwepo bei elekezi

GE2025 Mgombea Mwenza NCCR-Mageuzi: Wakulima watapanga bei ya mazao yao bila kuwepo bei elekezi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Evaline Munisi, ameahidi kuwa serikali itakayoundwa na chama hicho itawapa wakulima uhuru wa kujipangia bei ya mazao yao, bila kuwepo kwa bei elekezi kutoka serikalini.

Akizungumza leo Oktoba 9, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Chem Chem, Manispaa ya Tabora, Evaline amesema NCCR-Mageuzi itahakikisha sekta ya kilimo inakuwa na tija kwa kumwondoa mkulima katika utegemezi na changamoto za masoko.

Amesema endapo chama hicho kitapewa ridhaa kuongoza nchi, kitaanzisha viwanda vya tumbaku na mbao mkoani humo ili kurahisisha uchakataji na kuongeza thamani ya mazao hayo, hatua itakayochochea ajira na kuinua uchumi wa wananchi wa Tabora.

 
Back
Top Bottom