Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Bado sielewi Vigezo ambavyo vimetumika Kumfanya Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM.
Nchimbi hana na wala hajawahi kuwa na Ushawishi wowote kwenye siasa za ndani na hata kwenye Majukwaa ya hadharani, Hata alipofukuzwa na Magufuli ndani ya ccm kwa kuwa Team Lowassa hakuna aliyemsikitikia, Afadhali hata Sophia Simba wanaccm walimpigania, hii maana yake ni kwamba, Sophia Simba alimzidi mno kwa Umaarufu Nchimbi.
Mtu wa aina hii kumpeleka kwenye majukwaa ya kuomba kura ni sawa na kujibebesha Gunia la Misumali, Hata huu Mkutano wa Mkuu wa CCM ambao umeratibiwa naye kama Katibu Mkuu wa Chama, ndio mkutano mkuu wa ccm uliododa zaidi kuliko mikutano mikuu yote tangu kuanzishwa kwa chama hicho.
Soma Pia: Breaking News: - Uchaguzi 2025 - CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025
Naitabiria CHADEMA kampeni nyepesi zaidi kuliko Uchaguzi wowote tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi Nchini Tanzania, kazi ni kwenu Chadema, labda itumike tu mbeleko ya dola, lakini Je dola itakubali kutumika kubeba maji kwa kutumia Tenga? Je Pipa litajaa?