Mgombea Ubunge ashawishi Kamati ya Siasa ya Wilaya kuwakata majina yote watia nia ya Udiwani wasiomuunga mkono

Puma yetu

Senior Member
Joined
Sep 23, 2016
Posts
111
Reaction score
125
Katika hali isiyokuwa ya kawaida aliyekua mbunge jimbo la Singida Magharibi ndugu Elibariki Kingu alishawishi kamati ya siasa ya Wilaya kuwakata majina wale wote waliotia nia ya kugombea udiwani CCM wasio muunga mkono yeye.

Sasa watia nia hawa wa udiwani wanasubiri majina yao yakatwe watinge Dodoma kuilalamikia kamati ya siasa ya Wilaya pamoja na ya mkoa na kuzishtaki kwa Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashir Ally pamoja na Mwenyekiti wa Chama Taifa Dkt. John Pombe Magufuli.

Najaribu kuwaza kwa mbali, kwanini huyu aliyekua mbunge amekua katili kiasi hicho kwa wenzake?

Tazama video hiki.

Your browser is not able to display this video.
 
Huyu jamaa alikuwaga smart sana alipokuwa mkuu wa wilaya sijui kawaje alipopata ubunge?
 
Kwan ana nguvu gani ya ushawishi
 
Mgombea anapata wapi mamlaka ya kuiambia kamati ya siasa ikate majina ya wagombea wenzake?
 
Huyu dawa yake ni spana Spana.Kwanza hana influence kwa wananchi na hawampendi kwa uongo wake wa kutotimiza ahadi zake
 
Huyu ni jàmbazi wa siasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…