Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kakonko kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Damas Philbert Damas, amemuombea kura mgombea ubunge mwenzake wa chama cha ACT Wazalendo wa jimbo hilohilo, Olaf Kaboboye, katika tukio lililofanyika Kata ya Katanga, Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma
Tukio hilo lilitokea Jumatatu, Oktoba 6, 2025, wakati Kiongozi wa ACT Wazalendo mstaafu, Zitto Zuberi Kabwe, alipokuwa akimnadi Kaboboye mbele ya wananchi wa eneo hilo
Olaf Kaboboye, ambaye ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, ni miongoni mwa wagombea wanaowania nafasi ya ubunge kupitia ACT Wazalendo katika mkoa wa Kigoma
Wakati wa mkutano huo, Damas alionesha nia ya ushirikiano kwa lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha umoja na demokrasia katika kipindi cha kampeni na azma ya pamoja ya kuiondoa CCM madarakani