The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mgombea ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dickison Lutevele maarufu kama Villa, amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29, akiwahakikishia kuwa hali ya usalama itaimarishwa ili kila mtu ashiriki uchaguzi kwa amani.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Bumilayinga 6 Oktoba 2025 Villa alisema kuwa serikali ya CCM imejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu na kila mwananchi anapata nafasi ya kuchagua viongozi wake kwa uhuru.
Aidha alieleza mafanikio yaliyopatikana chini ya serikali ya awamu ya sita, ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwemo kupatikana kwa mbolea za ruzuku , elimu bure kwa watoto wa shule ya msingi hadi sekondari, na ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma.
Villa aliahidi kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo, akipewa ridhaa ya kuwa mbunge, atahakikisha wazee wanatibiwa bure na kwa heshima, na atakuwa karibu na wananchi ili kusikiliza na kufuatilia matatizo yao kwa ukaribu zaidi.