McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Wakuu,
Katika mkutano wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Siha, mgombea ubunge Katika jimbo hilo kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mdoe Yambazi Azaria, alikua ni miongoni mwa mamia ya wananchi waliojitokeza Katika Mkutano huo huku akimpongeza mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mdoe alisema hana pingamizi kwa utekelezaji wa Rais Samia, akibainisha kuwa hata katika video zake za kampeni amekuwa akimpa sifa.
"Mimi namkubali, hata kwenye video zangu nimemtoa sana kumsifia. Kwa hiyo kwa Mama Samia sina tatizo," alisema Mdoe mbele ya hadhira.
Alipoulizwa sababu ya kuhudhuria mkutano wa CCM licha ya kuwa si mwanachama wa chama hicho, Mdoe alijibu kwa kusema siasa siyo uadui.
"Siasa si uadui. Hata wapinzani wangu wakija kwenye mikutano yangu siwazuii. Kuna mambo wanaweza kujifunza. Ndiyo sababu na mimi nimekuja hapa," aliongeza.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa CCM wilayani Siha, mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi, alimnadi mgombea ubunge wa chama hicho jimboni humo, Dkt. Godwin Mollel, huku akieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali katika kuboresha huduma za afya kwenye jimbo hilo