The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mgombea Ubunge Jimbo la Tabora mjini kupitia Chama cha Mapinduzi Hawa Mwaifunga leo Oktoba 7,2025 ameendelea na mikutano ya Kampeni kusaka kura za kuwa Mbunge wa Tabora mjini.
Mwaifunga akiwa katika kata ya Uyui amewataka Vijana kuchangamkia fursa za ajira katika viwanda ambavyo vitajengwa katika Jimbo la Tabora mjini kama ambavyo ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2025/30 ya Chama cha Mapinduzi inavyosema, Mwaifunga amesema kuwa tatizo kubwa kwa Vijana ni Ulevi katika masaaa ya kazi,
Mbali ya fursa za kiuchumi Mwaifunga amewataka Wazazi wa kata hiyo kuwekeza kwenye kutoa Malezi bora kwa Watoto wa kiume kutokana na kuvunjika kwa maadali na vitendo vya ushoga kuongezeka katika Jamii.