McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Wazee wa kimila wa kabila la Waluguru, Kata ya Mlali wilayani Mvomero mkoani Morogoro, wamefanya matambiko maalum ya kimila kwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mvomero kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Sara Msafiri na Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, Frank Mwananziche, wakidai ni kwa ajili ya kuwalinda dhidi ya husuda na maadui wa kisiasa.
Khadija Abdallah Kiima, mmoja wa wazee wa kimila, alisema tambiko hilo ni sawa na dua ya kuwatakia baraka na ushindi wagombea hao, akieleza kuwa wanawaona kama watoto wa Mlali wanaotarajiwa kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii yao.“Hawa Sara na Frank ni watoto wetu, wazaliwa wa hapahapa.
Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Mvomero, Sara Msafiri, alisema matambiko hayo yamempa nguvu zaidi kuanza kampeni, akiahidi kuendesha siasa za kistaarabu, kushirikisha makundi yote ndani ya chama na kuwaunganisha wanachama wa CCM ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Naye Mgombea Udiwani wa Kata ya Mlali, Frank Mwananziche, alisema anaamini baraka hizo za wazee zitamuwezesha kuendesha kampeni zenye mshikamano na kuibua mwelekeo mpya wa maendeleo kwa wananchi wa Mlali, hususan vijana na wakulima wa eneo hilo.
Kampeni kubwa za CCM Wilaya ya Mvomero zinatarajiwa kufunguliwa rasmi Septemba 7, 2025 katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Mzumbe, ambapo wagombea wa chama hicho wataeleza wananchi sera na ilani ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu.