Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,984
Ndugu wadau,
Kuna taarifa nimekuwa nikizipata siku za hivi karibuni kutoka Wilayani Serengeti kwamba mgombea ubunge wa jimbo la Serengeti kupitia chama cha CCM aliandika barua ya kutaka kujitoa kwenye kinyang'anyiro baada ya kukutana na hali ya kutokubalika kwa wapiga kura wa jimbo hilo, kutokana na moto wa Mwl. Marwa Ryoba mgombea wa chama cha CHADEMA. Baada ya kufikisha barua hiyo kwa viongozi wa ccm wilaya na kufanyika mawasiliano na ccm makao makuu, alionywa kwamba asithubutu kufanya jambo hilo kwani angekiaibisha chama na akatishiwa kuchukuliwa hatua kali na chama kama angetekeleza nia yake hiyo.
Inasemekana sababu kubwa ya kutokubalika kwake ni matokeo ya kura za maoni ndani ya chama hicho, ambapo inadaiwa Dk Kebwe alitumia mbinu za kimafia kumuangusha Dk Wanyancha aliyekuwa mbunge 2000-2010.Hali hiyo imesababisha kuzomewa na wananchi kila anapofanya kampeni au hata anapopita mitaani, na hivyo kutembea na askari polisi 6-10 kila anapokuwa kwenye shughuli za kampeni.
Kama kuna mwenye habari zaidi naomba atufahamishe.
Nawasilisha.