Elections 2010 Mgombea Ubunge wa CCM Serengeti "abwaga manyanga"

Elections 2010 Mgombea Ubunge wa CCM Serengeti "abwaga manyanga"

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2008
Posts
10,565
Reaction score
7,984
Ndugu wadau,
Kuna taarifa nimekuwa nikizipata siku za hivi karibuni kutoka Wilayani Serengeti kwamba mgombea ubunge wa jimbo la Serengeti kupitia chama cha CCM aliandika barua ya kutaka kujitoa kwenye kinyang'anyiro baada ya kukutana na hali ya kutokubalika kwa wapiga kura wa jimbo hilo, kutokana na moto wa Mwl. Marwa Ryoba mgombea wa chama cha CHADEMA. Baada ya kufikisha barua hiyo kwa viongozi wa ccm wilaya na kufanyika mawasiliano na ccm makao makuu, alionywa kwamba asithubutu kufanya jambo hilo kwani angekiaibisha chama na akatishiwa kuchukuliwa hatua kali na chama kama angetekeleza nia yake hiyo.
Inasemekana sababu kubwa ya kutokubalika kwake ni matokeo ya kura za maoni ndani ya chama hicho, ambapo inadaiwa Dk Kebwe alitumia mbinu za kimafia kumuangusha Dk Wanyancha aliyekuwa mbunge 2000-2010.Hali hiyo imesababisha kuzomewa na wananchi kila anapofanya kampeni au hata anapopita mitaani, na hivyo kutembea na askari polisi 6-10 kila anapokuwa kwenye shughuli za kampeni.

Kama kuna mwenye habari zaidi naomba atufahamishe.

Nawasilisha.
 
Inasemekana sababu kubwa ya kutoubalika kwake ni matokeo ya kura za maoni ndani ya chama hicho, ambapo inadaiwa Dk Kebwe alitumia mbinu za kimafia kumuangusha Dk Wanyancha aliyekuwa mbunge 200-2010.Hali hiyo imesababisha kuzomewa na wananchi kila anapofanya kampeni au hata anappita mitaani wananchi humzomea.

Wapigakura wa mwaka 2010 siyo wale wa 1995
 
hii itakuwa habari njema. Lakini kama upepo ni mbaya hata asipojitoa bado wananchi watamtosa tu. Jamaa wa mkoa wa Mara huwa hawapendi upuuzi. "Amang'ana kasarikire mura"
 
Bado moto unawaka ndio watashangaa sana kuona mambo yanaenda kama hivi safi CHADEMA
 
na yule mama wa kawe namshauri afuate nyendo za mwenzake wa serengeti.
 
hata ngazi ya urais ingefaa ajiuzulu kulinda heshima ya chama chake ccm
na yeye mwenyewe .
 
wengi wamebadilika, tofauti na zamani
....na wanaendelea kubadilika kila siku, na hasa wanaposikia sera na ahadi za vyama, na utumbo wa waliopo madarakani.
 
hata ngazi ya urais ingefaa ajiuzulu kulinda heshima ya chama chake ccm
na yeye mwenyewe .
Ahahahahahahahahaaaaah atakuwa ameweka rekodi ya aina yake :biggrin1::biggrin1::biggrin1:
 
hata ngazi ya urais ingefaa ajiuzulu kulinda heshima ya chama chake ccm
na yeye mwenyewe .

Dr. Slaa anasubiriwa kwa hamu sana na wapiga kura wa Serengeti.
Chadema wasije wakafanya makosa kumchelewesha Rais mtarajiwa kuingia mjini Mugumu.
JK alifika Mugumu akiwa amechelewa sana na hakupata hata muda wa kutosha kusalimia wananchi, kitendo hicho kimewakera wengi.
Sasa hivi kila mtu ana hamu ya kumuona na kumsikia "Live" Dr. Slaa ndani ya mji wa Mugumu kabla ya kutoa hukumu ya haki 31/10/2010.
 
haya majigambo yatawafanya wengi kulia itakapofika 31 octoba siku mbili kabla ya kuapishwa kwa kikwete kuwa Rais.
 
Habari nilizonazo ni kwamba mgombea wa CCM anakubarika tofauti na maelezo tunayopewa hapa
 
udaku,udaku,udaku mura...

Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join DateThu Oct 2010Posts2Thanks0Thanked 0 Times in 0 Posts


Bisha hodi kwanza, usiingie kichwakichwa kama vile kichakani!!
 
Habari nilizonazo ni kwamba mgombea wa CCM anakubarika tofauti na maelezo tunayopewa hapa

Sasa mama porojo, kama sio porojo kama lilivyo jina lako, ilikuwaje Dk. Kebwe akaandika barua ya kujitoa kwenye kinyang'anyiro?
 
haya majigambo yatawafanya wengi kulia itakapofika 31 octoba siku mbili kabla ya kuapishwa kwa kikwete kuwa Rais.

Kwa waliozoea kuiba kura lazima watalia, kwa kuwa mwaka huu haibiwi mtu.
Lakini kwa wale wanaotafuta kura zao kwa haki hata wakishindwa wanachukulia kawaida tu.
 
Habari zaidi zinasema kuwa hata ule mgombea wa Jimbo la Nzega naye kajitoa na hafanyi tena kampeni kwani kila anapopita ni Bashe Bashe!!!!

Bado Jk nadhani hatafika tarehe 25 oct atakubali matokeo...... Mzee amechoka jamani mbaya.. jana nimemsikia akiongea kule kigoma na kama kawaida yake amejaza watoto tu.... Mzee hali yake taabani..

Slaa mwendo mdundo!!!
 
Back
Top Bottom