Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Hivi unamjua Lema kweli hadi ukafikia conclusion kuwa hakufanya hilo na ni njama za mpizani wake??? Yaleyale ya wanaCCM waliokuwa wakikamatwa na takukuru halafu utetezi wao pekee ni kuwa ni njama za wapinzani wao???
Heshima kwako Omarilyas
Bahati mbaya wachangiaji wengi hawapendi kuangalia pande mbili za shilingi wako tayari kutetea ujinga kwakuwa mkosaji ni mtu wao.Lema hakuwa na sababu za msingi kumtisha msimamizi wa uchaguzi eti akishindwa kwenye uchaguzi atamuua.Bahati mbaya Lema katamka maneno haya mbele ya watu kibao ushahidi upo tena usiokuwa na shaka subirini kesi itinge mahakamani mtashangaa jinsi alivyo mjinga.Nasisitiza tena na tena kwaajili ya kuweka rekodi sawasawa Lema anaponzwa na ukosefu wa elimu,laiti Lema angesoma vizuri angekuwa mwanasiasa mzuri pengine miaka ijayo angefaa kugombea urais.Jamani tuumize akili kidogo ili tuweza kupata majibu sahihi,kwanini Lema alidai ana Advance Diploma wakati anajua wazi hana hata sifa za kujiunga na kozi hiyo hana.Alikuwa na sababu gani za msingi kudanganya ilihali anajua anaweza kushtakiwa kwa kosa la kughushi elimu asiyokuwa nayo.
Namfahamu sana kaimu mkurugenzi wa jiji Bwana Estomie Chang'a tangu akiwa Assistant administrative officer na baadae Senior Administrative Officer ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.Ni mtumishi wa serekali kama walivyo watumishi wengine wengi wa serekali kapelekwa pale baada ya mkurugenzi wa zamani kuboronga na si kama watu wengi wanavyodhani kahamishwa kwaajili ya kuandaa mazingira ya ushindi wa Mama Batilda.Hisia za kijinga na propaganda za Lema zinawaanda wapiga kura wake kukata tamaa kabla ya uchaguzi kufanyika.Serekali ina haki ya kumwamisha,kumwadhibu,kumfukuza kazi mtumishi yoyote kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo.Uhamisho wa mkurugenzi umeleta tafrani kiasi hata mimi nilianza kuamini lakini baada ya kuzungumza na baadhi ya watumishi manispaa [jiji] walishangaa mkurugeni kuhamishwa badala ya kufukuzwa kazi na kushtakiwa.