Ilivyokuwa: Lema alikuwa anatoka kwenye mkutano wa kampeni ambao ulifanyika Levorosi na kufungwa saa 12:4 jioni basi wakati Lema anaondoka wapenzi wa CHADEMA wakaungana msafara wakimsindikiza huku wakiwa na mzuka wa ajabu yaani ni honi na miluzi ndiyo ilikuwa imeshamili inakadiliwa magari zaidi ya 30 hivyo ikawa kama kwamba anafanya maandamano na kusababisha jam kama unavyo ujua mji wa arusha walipo fika idara ya maji karibu na Posta Meru polisi walianza kuwa sihi wasitishe hayo maandamano kama walivyo yatafasili, hawakutii amri hiyo wakidai hayo siyo maandamano bali ni msafara wa kumsindikiza mbunge wao nyumbani na walioji kwani msafara mwisho gari gapi? walipo fika mnara wa mwenge ndiyo polisi walipoongezeka nakublock nakuanza kuamrisha baadhi ya magari yaelekee Kaloleni magine centre imradi wawasambaratishe kuna baadhi walikadi amri ya polisi ndipo polisi wakaanza kuwa telemsha kwenye magari yao nakuwapiga kuna jamaa aliumia sana hivyo lema aliamua kwenda polisi kuchukua PF3 ili jamaa akatibiwe alipofika pale reception (Polisi) alimkuta kamanda Basilio alimwambia anamtafuta ndipo alipomwambia ningilia kwa wapi nipite juu ya meza au nizunguke akamwambia zunguka Lema akazunguka, alipofika aliopo kamanda Basilio alimwambia nimekuja kwajaziba, Basilio akamwambia "nitakupiga" Lema akamwambia unataka unipige makofi au risasi kama ni risasi piga hapa akimwonyesha sehemu ya kupiga huku akivua shirt na kushika kwenye moyo akiimanisha ndiyo sehemu sahihi ya kupigwa kwa risasi ndipo Basilio nadhani kwa kuona anadhalilishwa maana hayo yote yalitokea mbele ya polisi na wananchi akaamrisha Lema awekwe ndani walimtaka aandike maelezo kabla hajaingia ndani Lema aligoma akitaka wakili wake (Amani) awepo ilibidi awekwe ndani huku wakimsubilia wakili, watu walijazana Polisi wakitaka kujua nini kimetokea kwa mbunge wao wakafukuzwa walitawaywa kwa virungu lakini ilipotimu saa 4:30 watuwalikuwa wamejaa tena wakitaka kujua kama Mbuge wao atatoka au laah, polisi walikuja na kuwaambia wakae mita 200 kutoka kituo cha polisi watu wakagoma kukatokea purukushani safari hii polisi walishinda tena kwani watu walipanda kwenye magari yao na kuondoka mahali hapo na kuja kusiama maeneo ya Arusha City park
.
Bw Godbless Lema alitolewa usiku huo huo