wafuasi watano wa chama cha mapinduzi akiwemo mdogo wa mbunge wa jimbo la kibakwe wilayani mpwapwa wametiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mfuasi mmoja wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) yaliyotokea katika kijiji cha pwaga wilayani humo.
Tukio hilo lilitokea siku ya alhamisi tarehe 28/10/2010, inadaiwa katika tukio hilo wafuasi wa chadema walikuwa wakitoka kwenye mkutano wao na wakapita karibu na eneo ambalo ccm pia walikuwa wakifanya mkutano, kisha ccm kuona wafuasi wa chadema wanashangilia wakaanza kuwashambulia na katika tukio hilo mtu mmoja aliyekuwa amepanda powertiller alivutwa na kuanguka kisha akaanza kushambuliwa na wafuasi wa ccm mpaka mauti yalipomkuta
watuhumiwa wametiwa mbaroni na upelelezi kamili juu ya tukio hilo unaendelea
ikumbukwe jimbo la kibakwe upinzani kati ya ccm na chadema ni mkali mno.