Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 20,694
- 32,527
Habari wanaJF, leo nipo hapa kumshauri mgombea ubunge jimbo la Ubungo, ndugu Boniface jacob jinsi ya kubadilisha mikakati ili aweze kulibakiza jimbo la Ubungo chini ya CHADEMA. Watu wengi wa Ubungo wanakufahamu hivyo yakubidi uanze pale ulipoishia kwenye umeya. Ulifanya mazuri na wana Ubungo wanaonekana wana imani na wewe, ila punguza kidogo siasa za kujikweza.
Pili; yakupasa uongeze spidi iwe mtaa kwa mtaa hata kila baada ya siku 3, spidi ya mwanzoni ilikuwa nzuri sana ila sasa hivi ni kama umepunguza hivi, pengine ni kutokana na masuala ya kiuchumi kutokukaa vizuri.
Ni ukweli usio na shaka kuwa kuna wanachama wa CHADEMA hapo Ubungo hawakutaki, pengine ni kutokana na fitna + wivu walionao kwao au pengine ni kutokana na yale yaliyotokea kwenye kura za maoni, yote kwa yote hawa pia ni watu muhimu kwako kipindi hiki(si kila adui ni wa kushambuliwa).
Nikutakie kampeni njema ila fanyia kazi hayo, utafika mbali sana. Chini hapa ni picha ikionyesha Boniface Jacob akihutubia MAELFU YA WATU kwenye mkutano wake wa kampeni.