Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge wa CHADEMA Karagwe, Adolf Mukono, Wagombea udiwani Kata za Chanika na Kituntu wakamatawa na Jeshi la polisi

Huu muda uliobaki wasitegemee majukwaa ni mwende wa nyumba kwa nyumba na masokoni, stand, na hata siku za vikundi vya kina mama wawaulize wake zao waende kuomba kura kimya kimya, na wale wa vijijini hata visimani na mabombani mbona njia ziko nyingi bila hata mkutano wa hadhara kama wa mgombea mwenye kibali.
 
Kampeni ya waziwazi ni hivi! Sipati picha kura ya sirini matokeo yatakuwake!!

Mbona kama tunapoteza tu muda na rasilimali ilhali kuna watu wana maamuzi juu ya kipi kitokee!!
 
Polisi wanatumika kindezi sana
Naiona future ya IGP Sirro ndani ya kuta za gereza. Kwa nini lakini huyu Mseminari anakubali kuharibu uzee wake kama mstaafu kwa amri ambazo angeweza kuzikataa kwa kujiuzulu kwa heshima yake?

Hivi anakubali wanae na wajukuu huishi kwa huzuni kwa kumuogopa mwanaume mwenzie tena asiye na historia yeyote ya ushupavu?
 
Kiongozi umeelewa kilichoandikwa? Ama umeamua kujumlisha ki itikadi?
Hapa umeelewa nini?


"Tumewakamata baada ya kupata malalamiko kutoka upande wa CCM wakidai kwamba Chadema hawana ratiba ya kufanya kampeni zozote katani Chanika. Tulipomwuliza Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya akatuthibitishia hilo. Nasi tumeona tuchukue hatua ili kuepusha shari."
 
Hivi kwani bila polisi kutumika vibaya uchaguzi hautaenda? mbona awamu nyingine hautukuwahi kushuhudia nguvu nyingi zikitumika namna hii. Tutashuhudia mengi sana
 
Kwa hiyo polisi wanafuata maelezo ya CCM, CHADEMA wakiropoti CCM kuvunja taratibu polisi wanaufyta,kweli haki inagharama
 
Habari iliyo andikwa imejumuisha mambo mengi vikirishi, kwa mfano kitendo cha polisi kung'oa bendera za chadema, polisi kuongozana na m/kiti wa ccm kuwakamata wanachama na viongozi wa chadema, barua mbili za NEC zenye maelezo na anuani tofauti nk.
Sasa unapo chomoa kipengele kimoja na kukitolea hukumu, ndio nikauliza umeelewa kilicho andikwa, ama umejumlisha ki itikadi?

Lakini kipengele ulicho kichomoa kina utata bado. Chadema wanatumia barua iliyo ruhusu kutoka NEC Dodoma, na polisi wanatumia barua iliyo kataza kutoka NEC Dar. Nani yuko sahihi kati yao? Mimi na wewe tunapata wapi haki ya kuhukumu kwa mujibu wa barua za aina hiyo?
 
Ile clip ya Tume iliyovuja ilikuwa inadai walikosea kumpa barua mgombea udiwani wa Kata ya Chanika, wakajikuta barua imeshapokrlewa aidha walilenga kumchomoa kwenye kinyanganyiro.
 
Polisi usalama wa taifa Mkuruvenzi wote ni CCM itakuwaje tume iamrishe Wagombea warudishwe harafu kuwena baruwa nyingine iseme hawajareshwe charles mahera wa kutupwa kwenye tanuru la moto maana amejiandaa kusababisha vita nchk hii
Mpaka wameungana wote na bado tumewsshinda kila mahali. Kwa Nguvu za Mungu tutawashinda tu.
 
Polisi wako sahihi, chadema ni waongo na wazushi kama ilivyo desturi yao
 
Hawa watendaji wanamhujumu JPM kwa makusudi huku wakifikiri wanajipendekeza .
Piga spana majinga hayo ya ccm kwenye sanduku la kura.
 
Huyo afisa usalama wa taifa wilaya anahusika vipi na mambo ya uchaguzi, ngoja atashughulikiwa baada ya lissu kuapishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…