Elections 2010 Mgombea udiwani CHADEMA kata ya Kati apata kipondo Korokoroni

Elections 2010 Mgombea udiwani CHADEMA kata ya Kati apata kipondo Korokoroni

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Mgombea udiwani kwa tiketi ya CHADEMA kata ya Kati mjini Arusha Bwana Simba aumizwa vibaya kituo cha polisi wilaya ya Arusha.Bwana Simba alikamatwa na polisi kwa sababu ambazo bado sijazithibitisha.

Bwana Simba alishambuliwa vibaya na watuhumiwa wenzake aliowakuta wamewekwa rumande katika kituo cha polisi hadi kuzimia na baadae kukimbizwa hospital ya mkoa wa Arusha [Mt meru Hospital] kwa matibabu.
 
:mad2:hizo ni hila za CHAMA CHA MABWANYENYE...... mwaka huu wao watasoma namba.
 
Wameshaanza hujuma zao na mungu yupo tu

kijana atapona na kura atapata za kutosha
 
Please tunataka kujua sababu ya kupigwa vibaya hivyo na ilikuwaje kuwa rumande
 
jamaa huyo ambaye ni mgombea wa udiwani Chadema alisema akipata udiwani atafuta kodi zote ikiweko ya masoko pale Arusha (Source, slaa kwenye kampeni za moshi). Binafsi naona serikali na polisi ilichofanya ni sawa tu kumsweka ndani. sasa kama wewe unaahidi utafuta kodi utaendeshaje kata yako? jimbo lako? Nchi yako? yaani hawa ni wababaishaji tu hamna lolote.
 
Mgombea udiwani kwa tiketi ya CHADEMA kata ya Kati mjini Arusha Bwana Simba aumizwa vibaya kituo cha polisi wilaya ya Arusha.Bwana Simba alikamatwa na polisi kwa sababu ambazo bado sijazithibitisha.

Bwana Simba alishambuliwa vibaya na watuhumiwa wenzake aliowakuta wamewekwa rumande katika kituo cha polisi hadi kuzimia na baadae kukimbizwa hospital ya mkoa wa Arusha [Mt meru Hospital] kwa matibabu.

wewe mwenyewe unayeripoti hii habari unajua ukweli sana tu na ndo maana umekwepa kueleza ukweli kuwa jamaa alitangaza kufuta kodi zote, sasa hata kama wewe ndo ungekuwa unasimamia serikali ungefanyeje? ungeacha mtu wa aina hii aendelee kukampeni? usalama wa taifa unafanya nini
 
Back
Top Bottom