GE2025 Mgombea Udiwani Ihumwa kwa madai ya kutojua kusoma na kuandika

GE2025 Mgombea Udiwani Ihumwa kwa madai ya kutojua kusoma na kuandika

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Aliyekuwa Mgombea Udiwani Kata ya Ihumwa Jijini Dodoma Musa Sajilo ambaye jina lake limeenguliwa kwa madai ya kutojua kusoma na kuandika amekiomba Chama cha Mapinduzi (CCM) kuingilia kati suala hilo kwa madai lina hujuma.

Akizungumza na Vyombo vya Habari Agosti 16 Jijijni Dodoma, ameeleza kuwa alichukua fomu na kujaza wakiwa wagombea 10 majina yakarudi matatu ambapo yeye ndie aliyeongoza kwa kupata kura175.

Sajilo amebainisha kuwa aliyemfuatia Edward Magawa ambaye pia aligombea nafasi hiyo alipata kura 130 huku mgombea wa tatu Mary Hoya akipata kura 7.

🗣"kinachonishangaza mbona wakati wa mchakato huo sikuambiwa sijui kusoma na kuandika baada ya kuchaguliwa ndio niambiwe sijui kusoma na kuandika hapa kuna kitu kinaendelea," Amesisitiza Musa

Aidha amebainisha kuwa tayari ameshaandika barua kwa uongozi wa CCM Taifa kupinga suala hilo.
Chanzo: Efm

Screenshot 2025-08-16 190613.png
 
Back
Top Bottom