GE2025 Mgombea Udiwani, John Ryoba Mrema anadi sera zake, asema watajenga kivuko katika Mtaa wa Kanga

GE2025 Mgombea Udiwani, John Ryoba Mrema anadi sera zake, asema watajenga kivuko katika Mtaa wa Kanga

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
Mgombea Udiwani katika Kata ya Kinyerezi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, John Ryoba Mrema (Wahenga aluminium) amesema endapo atachaguliwa kuwa diwani katika hiyo hatakuwa tayari kuona maturubai katika kipindi cha mvua kwenye bàadhi ya mitaa ikiwemo Mtaa wa Kanga.

WhatsApp Image 2025-09-19 at 11.29.14_de2d7b00.jpg

WhatsApp Image 2025-09-19 at 11.29.15_8f15fcb6.jpg

Wahenga ametoa kauli hiyo Septemba 18, 2025 katika mkutano wa hadhara wa kampeni zake uliofanyika katika kiwanja cha stendi ya zamani Kinyerezi.

Kauli ya Wahenga imekuja kufuatia matukio mbalimbali ya vifo yaliyoripitiwa kutokea katika Mtaa wa Kanga kutuatia kukosekana kwa vivuko hususani kipindi cha mvua.

"Katika utumishi wangu wa udiwani nisiingependa kuona maturubai ya misiba kwenye bàadhi ya makazi ya watu, Tumeingia makubaliano na TANESCO na TPDC tutajenga kivuko katika eneo lile ili watu waweze kuvuka vipindi vyote.

Mbali na miundo mbinu ya vivuko na barabara katika Kata hiyo Wahenga pia amezungumzia umuhimu wa wananchi wa Kinyerezi kuwa na maji ya uhakika katika misimu yote.

Mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Kanga, Rayra Soud amepongeza uamuzi wa mgombea huyo wa CCM kuja na mwarobaini wa kujenga vivuko kutokana na eneo hilo kuwasumbua kwa muda mrefu.

"Aaah ameniturahisha sana Wahenga nitampa tiki kubwa wahenga, Tumeteseka sana na lile korongo .

Naye mgombea Udiwani wa Kata ya Kimanga Jimbo la Segerea, Julius Lyimo amesema watu wa Kinyerezi wameokota dodo, Wahenga ni mpenda maendeleo, siri moja ya Wahenga ameshiba amejitosheleza yupo kwa ajili ya kuwatafutia nyie wananchi wake maisha"alisema Lyimo

Awali akizungumza katika hadhara hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Said Side alisema Wahenga alluminium ni kiongozi mzuri atatekeleza pale mwenzake aliyemaliza muda wake(Leah Mng'itu)alipoishia' alisema Said Side.
 
Sasa huyu ni mkurya au mchaga?
Ryoba,Mrema
 
Back
Top Bottom