GE2025 Mgombea udiwani kata ya Mwandege ACT apewe masharti mawili ama kupokea fedha au kupotezwa

GE2025 Mgombea udiwani kata ya Mwandege ACT apewe masharti mawili ama kupokea fedha au kupotezwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

kipati3

Member
Joined
Jul 13, 2025
Posts
23
Reaction score
17
Mtendaji wa kata katika ya Mwandege, jimbo la mkuranga Mkoa wa Pwani, Ally Mkawa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Luguruni B katika kijiji cha lugwadu, Shukuru Mkumba Wameingia katika tuhuma za kumshawishi na kumtisha Mgombea wa Chama cha Act Wazalendo katika kata hiyo Ramadhani Lugome kujitoa kuwania nafasi ya udiwani kwa ahadi ya kumpatia fedha kati ya Shilingi milioni 20-35

Ramadhani Lugome anasema alifuatwa kwa nyakati tofauti kati ya tarehe 14 na 17 mwezi huu, akitakiwa ajitoe kwenye kinyang'anyiro cha udiwani kwenye kata ya yake ya Mwandege kwa ahadi ya kupewa fedha vinginevyo ashuguhulikiwe kwa kupotezwa

Alisema awali akiwa katika eneo la Kivule jijini Dar esSalaam,alipokea simu ya mtu asiyemfahamu,akimshawishi kujitoa kwenye mchakato wa Uchaguzi kwa ahadi ya kumpatia kiasi cha shilingi milioni 20 kwa kuwa wahusika(hawakutajwa jina) wanahitaji uongozi katika kata hiyo.
Alieleza kuwa baada ya simu hiyo, siku iliyofuata ya Jumanne Septemba 16 mwaka huu aliitwa na Afisa Mtendaji wa kata ya Mwandege,Ally Mkawa, ambapo walikutana katika hoteli ya Green Tree iliyopo Tuangoma na katika kikaao hicho Mkawa aliambatana na jumla ya watu watatu waili kati yao akiwa hawafahamu na mmoja ni Shukuru Mkumba, kwa ajili ya mwendelezo wa mazungumzo ya kutakiwa kujitoa.

IMG-20250919-WA0009.jpg


“Mtendaji wa Kata si mgombea si mwanasiasa,aliniita tukakutana katika hoteli ya Green hapa Tuangoma,akaniambia nijitoe kwa ahadi ya kunipatia pesa,nikamwambia jana nilipigiwa simu na watu nisiowafahaamu wakaniahidi shilingi milioni 20 ninyi mmejipangaa vipi”alisema Lugome wakati akiongea na chanzo chetu cha habari
Alieleza kuwa baada ya majadiliano hayo Mkawa alimtaka aeleze kiasi kinachomstahili na kitakachofanyaa ajitoe kwenye kinyang’anyiro hicho cha Udiwani,ambapo alimueleza kuwa anapaswa kutafakari kabla ya kutoa jibu la kiasi anachostaahili.
“Kwa sababu ya mazingira niliyokuwepo wakati huo sikuwakatalia nikawaambia ninyi mliofikiria kuja kunishawishi ndiyo mna kiwango chenu tayari lakini mkitaka mimi niamue nipeti muda nikatafakari kwanza”alisema Lugome
Kwa upande wake afisa Mtendaji wa kata ya Mwandege Ally Mkawa,alipopigiwa simu na chanzo chetu cha habari kwa ajili ya kuelezeaa juu ya tuhuma hizo,alieleza kuwaa yupo kwenye kikao hawezi kuongea na atafutwe baadae.
Alipopigiwa kwa mara ya pili, MKawa alisikiliza hoja hizo na kueleza kuwa hayupo tayari kulizungumzia,huku Afisa Uchaguzi jimbo la Mkuranga,aliyefahamika kwa jina moja Ndugu Mwamfula akieleza kuwa taarifa hizo za mgombea udiwani kutakiwa kujiondoa hajazipata na kumtaka chanzo chetu cha habari afike ofisini kwake

Ally Mkawa mwenye shati jeupe pichani na shukuru mkumba mwenyekiti wa kitongoji mwenye vazi la suti nyeusi pichani

IMG-20250919-WA0010.jpg
 
Namaste namaste nawaambia 50 itapendeza malipo yafanyike kwa crypto. Ila uo mtego asizame mazima
 
Ramadhani Lugome anasema alifuatwa kwa nyakati tofauti kati ya tarehe 14 na 17 mwezi huu, akitakiwa ajitoe kwenye kinyang'anyiro cha udiwani kwenye kata ya yake ya Mwandege kwa ahadi ya kupewa fedha vinginevyo ashuguhulikiwe kwa kupotezwa
Takukuru ulisema matendo haya yaripotiwe kwao. Vipi wakikataa kuyapokea ndiyo maana mmeyaleta humu?
 
Udiwani unalipa sana kumbe,
malipo wanapewa nini, kiasi gani, na nini zaidi?
 
Fedha au kupotezwa?? Huko Mkuranga kama kwa Pablo kule Colombia PESA AU BUNDUKI

CCM IMECHOKA SANAA
 
Chukua 50M,
Hela ziwekwe kwenye acc ya UTT ya kampuni iliyofunguliwa kwa jina la babu wa mpwa wako 😂
 
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Luguruni B
Shukuru Mkumba
 

Attachments

  • IMG-20250919-WA0013.jpg
    IMG-20250919-WA0013.jpg
    188.5 KB · Views: 32
Fedha au kupotezwa?? Huko Mkuranga kama kwa Pablo kule Colombia PESA AU BUNDUKI

CCM IMECHOKA SANAA
Kwa tarafa za Leo
Madiwani wa upinzani WA kata zote za tarafa ya mkuranga wamefatwa na kutishwa au pesa

Ilo zoezi analiendesha MBUNGE WA Jimbo Abdallah Ulega
Lengo asipate Kura chache kama alivyopata 53% katika Kura za maoni za CCM
 
Kwa tarafa za Leo
Madiwani wa upinzani WA kata zote za tarafa ya mkuranga wamefatwa na kutishwa au pesa

Ilo zoezi analiendesha MBUNGE WA Jimbo Abdallah Ulega
Lengo asipate Kura chache kama alivyopata 53% katika Kura za maoni za CCM
Wajioganaizi waende kumwambia aachie jimbo au yeye apotezwe
 
Mtu mmoja anatishia madiwani wote na wanaoshindwa kujiunga ili wamshughulikie
 
Back
Top Bottom