PostGE2025 Mgombea Umeya H/Mji Bariadi aliyeteuliwa na CCM apigiwa kura nyingi za Hapana

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

KwetuKwanza

Senior Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
127
Reaction score
245
109600.jpg

Jana Chama cha mapinduzi CCM kimefanya uteuzi wa wagombea nafasi za Umeya, na wenyeviti katika Halmashauri za Wilaya, Miji, manispaa na majiji hapa nchini.

Katika Mkoa wa Simiyu, Halmashauri ya Mji wa Bariadi CCM iliteua jina moja tu la Zebedayo Lazaro Kingi ambaye ni Diwani kata ya Sima, kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.

Mapema leo Novemba 01, 2025 Madiwani wa CCM walikuwa wanapiga kura za maoni kudhibitisha jina hilo ili kuweza kugombea katika uchaguzi hapo kesho kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza Mgombea huyo amepigiwa kura nyingi za hapana ambazo ni 11 na kura za ndiyo 4 kati ya kura 15 za wajumbe wote ambazo zilipigwa.

Kwa mujibu wa baadhi ya madiwani walioshiriki uchaguzi huo (majina tunayahifadhi) wamedhibitisha matokeo hayo.
 
View attachment 3510038

Yah right. Sasa wanaCCM waneanza rebellion mapema hivi against Mwenyekiti. Kama hali ndoyo hii mwenzi wa kwanza tu itakuwaje baada ya miaka 2 ijayo?
 
CCM ni wa hovyo sana, mpaka umeya hauwaamini wanaccm wenzako mpaka umteue Dodoma kweli?
 
Back
Top Bottom