The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mgombea urais kupitia Chama cha Wakulima (AAFP), Kunje Ngombale Mwiru, amesema dhamira yake ya kufuga mamba Ikulu kwa ajili ya kuwala mafisadi si mzaha, bali ni mkakati mahsusi wa kupambana na ufisadi nchini.
Mwiru amesema wapo waliodhani kauli hiyo ni masihara ya kisiasa au porojo za kampeni, lakini akasisitiza kuwa ana uchungu mkubwa na mali za umma na hana nia ya kuyumbishwa katika mapambano dhidi ya wala rushwa.
Akizungumza na Nipashe Digital kuhusiana na ahadi hiyo, Mwiru amesema:
"Watu wanadhani ninatania, lakini kwenye masuala ya nchi hakuna utani. Nina uchungu na mafisadi wanaotafuna mali ya umma. Dawa yao ni kuwafanya wawe chakula cha mamba, ndiyo maana nimeahidi kuchimba bwawa Ikulu na kufuga mamba."
Ameeleza kuwa, iwapo atachaguliwa kuongoza nchi, serikali yake itaanzisha uchunguzi wa kina kwa kila atakayehusishwa na ufisadi, na wale watakaobainika bila shaka yoyote watakabiliwa na adhabu hiyo ya kipekee.
"Chama chetu kimeamua hivyo. Uchunguzi utakuwa wa haki na wa kina, na atakayethibitika, hatakuwa na kimbilio bali kuwa chakula cha mamba," amesema Mwiru.
Mbali na mapambano dhidi ya ufisadi, mgombea huyo ambaye anaendelea na kampeni zake mkoani Mtwara, ameahidi kuinua kilimo cha korosho kwa kupandisha bei ya zao hilo hadi kufikia shilingi 10,000 kwa kilo, ili wakulima wanufaike na kazi zao.