GE2025 Mgombea Urais ADA TADEA: Tutajenga jiji la Kiteknolojia. Litaitwa Bongo Selcom

GE2025 Mgombea Urais ADA TADEA: Tutajenga jiji la Kiteknolojia. Litaitwa Bongo Selcom

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha African Democratic Alliance (ADA - TADEA) George Gabriel Bussugu amesema kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, atahakikisha Tanzania inamiliki Satellite yake.

Akizungumza leo katika uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho zilizofanyika leo tarehe 14 Septemba 2025 katika viwanja vya Mbagala Zakheim Dar es salaam, Bussugu amesema atahakikisha Tanzania inakua kiteknolojia kwa kumiliki Satellite yake.

Aidha amesema kuwa katika kuhakikisha hayo yote yanafanyika Serikali yake itaanzisha kituo maalumu cha teknolojia Nchini ambocho kitaitwa Bongo Selcom City ambacho kitashughulika na Masuala yote yanayohusu teknlojia.


 
Back
Top Bottom