Mpepetaji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 346
- 213
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wilson Elias Mulumbe, amesema serikali ya ADC itahakikisha kila halmashauri nchini inakuwa na magari ya kisasa ya kuchimba visima vya maji, ili kumaliza kabisa tatizo la maji safi na salama kwa wananchi.
Mulumbe ametoa kauli hiyo leo Septemba 21, 2025, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Kingolwira, Mtaa wa Bomba la Zambia mkoani Morogoro, ambapo amebainisha kuwa tatizo la maji limeendelea kuwa kero kubwa kwa muda mrefu na serikali yake italipa kipaumbele cha juu.
Mbali na maji, Mulumbe ameahidi pia serikali ya ADC itaboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, nishati na miundombinu ya barabara kwa lengo la kuinua ustawi wa Watanzania wote.
Aidha, amesema wenyeviti wa serikali za mitaa kote nchini watawekwa kwenye mfumo wa malipo kwa kupewa mishahara, ili kutambua mchango wao katika kusimamia maendeleo ya wananchi.
Mulumbe amesisitiza kuwa ADC ina dira na mikakati madhubuti ya kuleta maendeleo ya kweli kupitia usimamizi bora wa rasilimali, uwazi katika utawala, na kuondoa mianya ya ubadhirifu wa mali za umma.