GE2025 Mgombea urais ADC: Serikali yangu itaweka satelaiti angani kuwanasa majangili na majambazi ndani ya maziwa

GE2025 Mgombea urais ADC: Serikali yangu itaweka satelaiti angani kuwanasa majangili na majambazi ndani ya maziwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Mgombea urais wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wilson Elias amesema endapo chama chake kitapata ridhaa ya kuongoza nchi, kitaweka satelaiti angani ili kudhibiti uhalifu unaofanyika katika maziwa ya Victoria na Tanganyika pamoja na mipaka ya nchi kwa ujumla.

Ahadi hiyo ameitoa Oktoba 23, 2025 alipofanya mikutano ya hadhara Kayenze na Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza, ikiwa ni mwendelezo wake wa kuomba kura mikoa ya Kanda ya Ziwa.

“Kilio cha wavuvi kinafanana kila mahali. Kumekuwa na majangili na majambazi ndani ya maziwa. Serikali yangu itaweka satelaiti angani eneo ambalo hakuna mtu anaweza kuona. Hii itaimarisha ulinzi kwenye maziwa pamoja na mipaka yetu yote, kwa hiyo maadui mwisho wao utakuwa umefika mtakapotuchagua ADC,” amesema Elias.

 
Bora uvumbue satellite na kunasa ruzuku.
 
Back
Top Bottom