GE2025 Mgombea Urais CUF awaonya wanaohamasisha Maandamano Oktoba 29, 2025

GE2025 Mgombea Urais CUF awaonya wanaohamasisha Maandamano Oktoba 29, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Gombo, amewatahadharisha wale wanaohamasisha maandamano siku ya kupiga kura, Oktoba 29, 2025, akisema nia yao ni kuichafua Tanzania huku wao wakiwa salama nchi za nje

Gombo ametoa kauli hiyo leo, Jumamosi Septemba 27, 2025, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mkoani Tanga, alipokuwa akitoa tathmini ya awamu ya kwanza ya kampeni zake alizozifanya katika mikoa 14 ya Tanzania Bara na Visiwani

“Wanaohamasisha maandamano hawako Tanzania. Wanataka kuona vurugu, wakati wao wako salama kwenye kumbi za starehe nje ya nchi. Watanzania wasikubali kutumika,” amesema Gombo

Mgombea huyo wa CUF amewasihi Watanzania wote kupuuza miito ya maandamano, badala yake wajitokeze kwa wingi katika vituo vya kupiga kura ili kufanya maamuzi ya kidemokrasia kwa njia ya amani

“Njia pekee ya kuiondoa CCM ni kupitia sanduku la kura, siyo kwa maandamano wala kususia uchaguzi. Watanzania wajitokeze kumpigia kura diwani, mbunge na rais kupitia CUF kwa ajili ya mabadiliko ya kweli,” amesisitiza

Soma pia GE2025 - Mgombea urais CUF aahidi elimu bure hadi Chuo Kikuu

1758978617023.png
 
Mgombea huyo wa CUF amewasihi Watanzania wote kupuuza miito ya maandamano, badala yake wajitokeze kwa wingi katika vituo vya kupiga kura
Lakini hajawahi kutetea NO REFORM NO ELECTION ana lalamikia kufanyika maadamano.
 
Back
Top Bottom