Mgombea Urais Kenya Anaswa na Bangi

b nyangi

Member
Joined
Apr 5, 2013
Posts
14
Reaction score
12
Marsabit, Kenya. Jeshi la Polisi nchini Kenya linamshikilia aliyekuwa mgombea kiti cha urais mwaka 2017, Jaffer Sora kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kilo 445.

Sora alikamatwa leo June 20, katika mji wa Marsabit akiwa amehiifadhi bangi hiyo kwenye gari yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mashariki, Esther Kihiko alisema Sora mwenye umri wa miaka 45 alikamatwa na bangi hiyo ikiwa imehifadhiwa katika tela ya gari yake aina ya Prado akiisafisha kutoka nchini Ethiopia.

Polisi nchini Kenya waliesma Sora alikamatwa jana katika kizuizi cha polisi baada ya askari waliokuwa wakifanya doria kumshuku na kumfanyia upekuzi.

“Bada ya upekuzi ilibainika alikuwa amebeba kiasi hicho cha bangi hivyo alimpeleka katika kituo cha polisi Marsabit,” ilisema

Kwa mujibu wa kamanda Kihiko mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani leo mara baada ya kukamilisha taratibu za kipolisi.
 


Cc: MK254 Unaona kazi hiyo???
 
Ndio maana 2pac alisema 'never get high on your own supply'. Huyu jamaa ni noma, yaani alikuwa anasafirisha mmea na hili gari lake hapa na trailer. Huku akiendeleza kampeni zake za kugombea kiti cha urais kwenye uchaguzi wa 2022! [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Ila ingekuwa miraa, angeruhusiwa. Kenya bhana, mwachieni jamaa.
 
Ila ingekuwa miraa, angeruhusiwa. Kenya bhana, mwachieni jamaa.
Ndio sheria hiyo, huwa haizingatii maoni wala hisia za watu. Hamna cha kuachia wala nini ukivunja sheria, unatupwa selo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…