Marsabit, Kenya. Jeshi la Polisi nchini Kenya linamshikilia aliyekuwa mgombea kiti cha urais mwaka 2017, Jaffer Sora kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kilo 445.
Sora alikamatwa leo June 20, katika mji wa Marsabit akiwa amehiifadhi bangi hiyo kwenye gari yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mashariki, Esther Kihiko alisema Sora mwenye umri wa miaka 45 alikamatwa na bangi hiyo ikiwa imehifadhiwa katika tela ya gari yake aina ya Prado akiisafisha kutoka nchini Ethiopia.
Polisi nchini Kenya waliesma Sora alikamatwa jana katika kizuizi cha polisi baada ya askari waliokuwa wakifanya doria kumshuku na kumfanyia upekuzi.
“Bada ya upekuzi ilibainika alikuwa amebeba kiasi hicho cha bangi hivyo alimpeleka katika kituo cha polisi Marsabit,” ilisema
Kwa mujibu wa kamanda Kihiko mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani leo mara baada ya kukamilisha taratibu za kipolisi.