Unamaanisha sie Civil servants tunatumia laki 2 kwa siku!doh,that is more like our monthly salary mh.
Au na wewe ni katika wale mnaoamini kila anayeendesha corola mjini anapokea mshahara wa milioni 20?!
kwa mindset hii ndio maana hii nchi rushwa haiishi,Mishahara midogo halafu unataka utumie laki 2 kwa siku!!haya masifuri muda si mrefu yatakuwa hayana maana. Huyo mgombea wa ubunge kutumia Laki 2 kwa siku is more than enough, Tatizo tumezoea wagombea wa ubunge kuwa kama wazazi, walezi katika kipindi chote cha uchaguzi.
wanatakiwa wagharamie logistics na other minor costs sio kulipia round za bar au kanga na vitenge
Mkuu Kimweri,
Naomba tuwe wakweli. Lita moja ya petroli/dizeli ni shilingi ngapi? Na je huyo mtu anahitaji magari mangapi kwa ajili ya kuandaa logistics za kampeni zake ikiwa ni pamoja na kufacilitate movement za kwake na wasaidizi wake? Au atakuwa anaenda kwenye kampeni kwa baiskeli au bajaji?
Kampeni ni pamoja na matangazo kwenye redio, magazeti na TV (esp. sehemu kama Dar ambapo wananchi wana access ya kusoma magazeti, kutazama TV na kusikiliza radio). Kitangazo kidogo kwenye gazeti ni zaidi ya hizo laki 2, je kuweka sera zake kwenye quarter/half/full page ataweza?
Hizo laki 2 hazitoshi kurusha tangazo kwenye TV hata kwa dakika moja.
Bado kuna kuchapisha vipeperushi pamoja na vitu vingine ambavyo vitakuwa vinamtangaza mgombea kwa wananchi pamoja na sera zake.
Bado unasema hizo laki 2 kwa siku zinatosha?
Tatizo la hiyo sheria ni kwamba hata kama mhusika ana hela zake pia inambana, haijalishi kwamba hizo hela ni zake ama zimetoka serikalini, kinachotakiwa ni ku-comply na hiyo sheria na pia aainishe sources za funds zake mapema ili wajue umezipata wapi na kwa njia ipi.
Tatizo siyo kwamba hela zinatolewa na serikali, tatizo ni kiwango. Kama mtu ana uwezo wa ku-raise funds kwa njia halali aruhusiwe kutumia kiwango kitakachomuzesha kujiuza kwa wapiga kura. Kitu ambacho walitakiwa kukiangalia kwa makini ni namna kwanza alivyopata hizo hela kama ni njia halali ama ni ufisadi; pili ni jinsi anavyotumia hizo hela, je anahonga ama anatumia kihali ili ku-facilitate kuuza sera zake kwa wananchi?
Pilau siyo kuuza sera, mafuta, mchele na sukari siyo kuuza sera; lakini kama anatumia hizo hela kwa kuuza sera zake na kujiuza yeye mwenyewe kwa wananchi kwa kutumia media mbali mbali za matangazo na kujiuza (mfano, vipeperushi, matangazo kwenye TV, radioni, kwenye magazeti na wakati mwingine hata t-shirt ama kofia ambazo zina kauli mbiu yake vinaweza kuwa vinamuuza candidate kwa wananchi).
The Act is tricky, itawashika wasio na connections/majina na walio na connections/majina watapeta. Victims wa kwanza zitakuwa ni nominations za CCM. Mwaka 2005 watu walilia na mchezo mchafu wa JK kwenye nominations, hakuna kilichofanywa na akaishia kupeta.
Chaguzi za Jumuiya za CCM zimejaa rushwa lakini kama mtoa rushwa ni "mwenzao", hakuna kitakachofanyika, ila kama mtoa rushwa siyo mwenzao basi lazima ashughulikiwe.