GE2025 Mgombea urais NLD, Doyo Hassan aahidi kurejesha reli ya Masasi-Dar es Salaam

GE2025 Mgombea urais NLD, Doyo Hassan aahidi kurejesha reli ya Masasi-Dar es Salaam

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mgombea urais kupitia Chama cha NLD, Doyo Hassan Doyo, amesema ikiwa wananchi watampa ridhaa ya kuwa rais serikali yake itarejesha reli ya kutoka Masasi (Mtwara) - Dar es Salaam ambayo ilisitisha shughuli zake 1972

Akizungumza Oktoba 21, 2025 katika mkutano wa kampeni na wananchi wa Wilaya ya Masasi amesema kuwa reli hiyo ilikuwa uti wa mgongo wa uchumi wa kusini, na kufufuliwa kwake kutachochea kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi

“Kupitia reli hii, wakulima wa korosho na mazao mengine ya biashara wataweza kusafirisha bidhaa zao kwa gharama nafuu hadi masoko makubwa ndani na nje ya nchi,” amesema Doyo

Ameongeza kuwa, uwepo wa reli utarahisisha biashara, ajira na uwekezaji, huku ukifungua fursa mpya kwa vijana na wanawake kupitia usafirishaji wa bidhaa, utalii, na huduma nyingine za kibiashara

Aidha, Doyo ameahidi kuanzisha Mkoa wa Kusini, utakaoundwa na Wilaya za Newala, Nanyumbu, Tandahimba, Nachingwea na Liwale, ikiwa atachaguliwa kuwa rais

1761229533026.png
 
Wanasiasa waongo sana,hii reli ilianzishwa na mwingereza baada ya vita ya pili ya dunia ili kuweza kusafirisha karanga zilizokua zinalimwa Nachingwea kwenda babdari ya mikindani,ili zipelekwe ulaya kwaajili ya kutengenezea mafuta ya kula.

Wamakonde na wamakua kwa akili zao finyu wakaihujumu ile reli na kung'oa mataruma.
 
Labda Wamakonde hawakuona faida yake?na kodi za muingereza zilikuwa juu? Iko sababu kwanini waliihujumu hio reli.
 
Back
Top Bottom