DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Hassan Almas, ameahidi kuwa iwapo chama chake kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi, serikali yake itatungua sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsi moja ndani ya siku 30 baada ya kuundwa kwa baraza la mawaziri.
Akihutubia wananchi mkoani Tabora katika mwendelezo wa kampeni za chama chake kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, Almas amesema NRA itasimamia ulinzi wa maadili na utamaduni wa Mtanzania kwa kuchukua hatua za haraka dhidi ya “tamaduni za kigeni” ambazo anadai zimeanza kupenya nchini.
Mbali na msimamo huo, mgombea huyo amesema serikali ya NRA pia itaboresha sera mbalimbali za kitaifa kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Ameahidi kuwasilisha sera mbadala zinazolenga kuongeza ustawi wa wananchi na kulinda heshima ya taifa.