tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Mgombea urais kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Kyara, amesema endapo atapewa ridhaa ya kuchaguliwa kuongoza nchi, serikali yake itatoa ajira milioni 10 ndani ya kipindi cha miaka mitano.
Kyara, ambaye aliambatana na mgombea mwenza wake Satia Mussa Bebwa, amesema mpango huo utatekelezwa ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa ajira nchini, hususan kwa vijana.
Ameeleza pia kuwa serikali ya SAU itarejesha heshima ya walimu kwa kuwapatia mazingira bora ya kufundishia, hatua itakayowezesha kuboresha kiwango cha elimu nchini.
“SAU inakwenda kuondoa unyonge kwa wananchi. Tunakwenda kutekeleza vipaumbele vyetu kwa ufasaha, ambavyo ni kilimo, afya na ajira,” amesema Kyara.
Umeme na Nishati Safi
Kyara ameahidi kuondoa gharama za umeme ili kuwawezesha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia, hatua itakayosaidia kulinda mazingira. Ameongeza kuwa serikali yake italeta kampuni ya kutengeneza majiko ya kisasa yenye teknolojia ya kuokoa nishati.
Fursa kwa Vijana
Amesema serikali ya SAU itazingatia zaidi ajira kwa vijana wa kiume, kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za uzalishaji na biashara.
Katiba Mpya na Ilani
Kyara amebainisha kuwa wiki ijayo watapiga hatua ya uzinduzi wa ilani ya chama hicho, huku akiahidi kurejesha mchakato wa Katiba Mpya itakayokubalika na wananchi.
Chanzo: Nipashe digital