Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wilson Elias Mulumbe, amesema miongoni mwa mikakati yake endapo atachaguliwa kuwa Rais ni kupunguza ugumu wa maisha kwa Watanzania na kuwezesha Watanzania wanaoishi nje ya nchi (diaspora) kupata uraia pacha ili kuchochea ukuaji wa uchumi.
Akiwahutubia Wananchi wa Mji mdogo wa Katoro, wilayani Geita, katika mwendelezo wa Kampeni zake leo, Mulumbe amesema hatua ya kuruhusu uraia pacha itasaidia kuongeza fedha za kigeni nchini, kupunguza makali ya kodi na kuimarisha ushiriki wa Watanzania waishio nje katika maendeleo ya taifa.
Ameongeza, “Lazima tufungue, tutengeneze vivutio vikubwa, ambavyo watu kutoka Rwanda na Burundi watakuja hapa kula bata, na vijana ambao mpo hapa niwahakikishie, mkinichagua kula bata itakuwa ni ‘Life style’. Vijana hawana furaha kwa sababu hawali bata, hakuna mzunguko wa fedha.”
Mgombea huyo pia ameeleza kuwa zaidi ya nchi 52 Barani Afrika tayari zimeruhusu uraia pacha na Tanzania inapaswa kuwa nchi ya 53 kuchukua hatua hiyo ili kuendana na mabadiliko ya dunia ya sasa