Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa ADC, Queen Cuthbert Sendiga ataja vipaumbele vyake vitatu

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Alliance Demokratic Party (ADC), Queen Sendiga amesema anaamini kuwa Watanzania watampigia kura za kutosha kumpa ushindi.

Amesema hiyo inatokana na uzuri wa vipaumbele vyake vitatu anavyovinadi ambavyo ni elimu, afya na kilimo.

Queen ni Naibu Katibu Mkuu wa ADC, mama wa watoto watatu na anajishughulisha na ujasiriamali.

Mgombea huyo mwenye shahada ya biashara, alisema jana kuwa anaamini kupitia vipaumbele vyake, ataweza kubadilisha maisha ya Mtanzania kutokana na mabadiliko ya sasa ya kidunia.

Alisema, tathmini aliyoifanya kwa zaidi ya miaka mitano akiwa ndani ya chama cha ADC na kupitia majukwaa ya harakati za haki za wanawake na watoto, ilitosha kuona ni wakati sahihi kwake kugombea urais wa Tanzania.

"Niliona kuwa tayari nimeshapata uzoefu wa kuweza kusimama mbele za watu wa kunadi sera zangu, kikubwa ili uweze kuwa kiongozi kwanza ni lazima ujue kitu gani cha kuongea na wananchi na wakati upi, binafsi nilijiona ninatosha kusimama katika nafasi hiyo na ndipo nikachukua uamuzi wa kugombea" alisema Queen.

Alisema licha ya changamoto anazozipitia, ukiwemo uhaba wa fedha, amepambana katika maeneo ambayo amefanikiwa kupita na sasa chama hicho kimeweza kutambulika kwa wananchi.

"Hadi sasa nimefanikiwa kufanya kampeni zangu katika mikoa nane ikiwemo mitano ya Zanzibar na kwa huku Tanzania Bara nimefanya mikutano yangu katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Pwani, kama Mungu akijalia kesho (leo) nitanadi sera zangu katika mkoa wa Lindi na katika kipindi cha siku tatu nitakuwa nimemaliza hadi mkoa wa Mtwara" alisema Queen.

Alisema anaamini hadi muda wa uchaguzi utakapofika, ataifikia mikoa yote na aliomba wananchi wajitokeze kwa wingi na kusikiliza sera zake .

Queen alisema Ilani ya chama hicho, imetoa kipaumbele kwa afya, kilimo na elimu kutokana na umuhimu wake katika maisha ya kila mwanadamu.

Kuhusu afya alisema atahakikisha kila mtu anapata tiba bora kwa gharama nafuu kulingana na kipato cha Mtanzania.

Kuhusu elimu, alisisitiza kuwa kila Mtanzania atapewa haki ya kuipata katika ngazi zote hadi chuo kikuu.

Queen alisema kwa upande wa kilimo, atahakikisha kuna upatikanaji wa pembejeo yakiwemo matrekta. Aliwataka vijana wapende kilimo.

Alisema anaamini Uchaguzi Mkuu utakuwa huru na wa haki na aliwasihi wagombea wahubiri amani, badala ya kuhamasisha vurugu.

"Tunagombea nafasi moja, yeyote ambaye atakuwa amejaaliwa na Mungu anaweza kuibuka mshindi, sioni sababu ya kutoa lugha zenye kujenga chuki miongoni mwa wananchi wetu, kikubwa tushiriki kampeni kwa amani na mwenye kushinda ashinde na mwenye kushindwa awe tayari kumuunga mkono mwenzake" alisema Queen.

Aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ihakikishe inasimamia haki na Jeshi la Polisi lihakikishe linasimamia mchakato mzima wa uchaguzi ili uweze kuwa wenye amani na utulivu.

Alisema anaamini katika uchaguzi huu, wananchi wengi watajitokeza na kupiga kura, kwa sababu elimu kuhusu umuhimu wa kupiga kura imetolewa kwa kiwango cha kutosha.
 
Umesomeka Rais mtarajiwa, ila itabidi ukubaliane na matokeo pia nakusifu kwa nafasi unayoipigania.

Kaza mama sisi walala hoi yetu macho tu tuone wapi mnatupeleka.

Kwenye nchi ya viwanda ama mafly over.
 
I love you Madam President. You are so Smart upstairs, so cute, wife material! I wonder ningeishi maisha ya raha kiasi gani kwa kuwa tu na mwanamke mwenye shahada ya biashara kichwani mwake na mzuri wa sura na umbo kama wewe!

You are a really Queen!!
 
i love you mtu hata picha hujaiona! kama ni jini je? mnakwama wap ufipa?
 
Queen huwa ninamuangalia mara nyingi kupitia luninga. Tatizo lako huwa unamuangalia mgombea wako tu magufuli muda wote. Uwe unasafisha macho!

Tangu Nchi hii ipate Uhuru, haijawahi kupata mgombea wa kike na mzuri kama Queen!! Hebu jiongeze basi halafu uje unipe na mrejesho.
 
daaah nmemuangalia, acha niweke comment yangu private
 
Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Alliance Demokratic Party (ADC), Queen Sendiga amesema anaamini kuwa Watanzania watampigia kura za kutosha kumpa ushindi.

Amesema hiyo inatokana na uzuri wa vipaumbele vyake vitatu anavyovinadi ambavyo ni elimu, afya na kilimo.

Queen ni Naibu Katibu Mkuu wa ADC, mama wa watoto watatu na anajishughulisha na ujasiriamali.

Mgombea huyo mwenye shahada ya biashara, alisema jana kuwa anaamini kupitia vipaumbele vyake, ataweza kubadilisha maisha ya Mtanzania kutokana na mabadiliko ya sasa ya kidunia.

Alisema, tathmini aliyoifanya kwa zaidi ya miaka mitano akiwa ndani ya chama cha ADC na kupitia majukwaa ya harakati za haki za wanawake na watoto, ilitosha kuona ni wakati sahihi kwake kugombea urais wa Tanzania.

"Niliona kuwa tayari nimeshapata uzoefu wa kuweza kusimama mbele za watu wa kunadi sera zangu, kikubwa ili uweze kuwa kiongozi kwanza ni lazima ujue kitu gani cha kuongea na wananchi na wakati upi, binafsi nilijiona ninatosha kusimama katika nafasi hiyo na ndipo nikachukua uamuzi wa kugombea" alisema Queen.

Alisema licha ya changamoto anazozipitia, ukiwemo uhaba wa fedha, amepambana katika maeneo ambayo amefanikiwa kupita na sasa chama hicho kimeweza kutambulika kwa wananchi.

"Hadi sasa nimefanikiwa kufanya kampeni zangu katika mikoa nane ikiwemo mitano ya Zanzibar na kwa huku Tanzania Bara nimefanya mikutano yangu katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Pwani, kama Mungu akijalia kesho (leo) nitanadi sera zangu katika mkoa wa Lindi na katika kipindi cha siku tatu nitakuwa nimemaliza hadi mkoa wa Mtwara" alisema Queen.

Alisema anaamini hadi muda wa uchaguzi utakapofika, ataifikia mikoa yote na aliomba wananchi wajitokeze kwa wingi na kusikiliza sera zake .

Queen alisema Ilani ya chama hicho, imetoa kipaumbele kwa afya, kilimo na elimu kutokana na umuhimu wake katika maisha ya kila mwanadamu.

Kuhusu afya alisema atahakikisha kila mtu anapata tiba bora kwa gharama nafuu kulingana na kipato cha Mtanzania.

Kuhusu elimu, alisisitiza kuwa kila Mtanzania atapewa haki ya kuipata katika ngazi zote hadi chuo kikuu.

Queen alisema kwa upande wa kilimo, atahakikisha kuna upatikanaji wa pembejeo yakiwemo matrekta. Aliwataka vijana wapende kilimo.

Alisema anaamini Uchaguzi Mkuu utakuwa huru na wa haki na aliwasihi wagombea wahubiri amani, badala ya kuhamasisha vurugu.

"Tunagombea nafasi moja, yeyote ambaye atakuwa amejaaliwa na Mungu anaweza kuibuka mshindi, sioni sababu ya kutoa lugha zenye kujenga chuki miongoni mwa wananchi wetu, kikubwa tushiriki kampeni kwa amani na mwenye kushinda ashinde na mwenye kushindwa awe tayari kumuunga mkono mwenzake" alisema Queen.

Aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ihakikishe inasimamia haki na Jeshi la Polisi lihakikishe linasimamia mchakato mzima wa uchaguzi ili uweze kuwa wenye amani na utulivu.

Alisema anaamini katika uchaguzi huu, wananchi wengi watajitokeza na kupiga kura, kwa sababu elimu kuhusu umuhimu wa kupiga kura imetolewa kwa kiwango cha kutosha.
Hicho ni chama cha upinzani au tawi la CCM?
 
Back
Top Bottom